Askari wa jeshi la magereza wakionyesha uhidari wao katika gwaride, picha hii ni ya maktaba haiusiane na tukio hili.
ASKARI magereza mwenye cheo cha Koplo amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kubainika
kuwalawiti kwa siku moja vijana wawili wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18
na 20.
Tukio la kuwalawiti vijana hao linadaiwa kufanywa
na askari huyo kati ya majira ya saa 7.00 mchana na saa 2.00 usiku katika moja ya nyumba za
kulala wageni (jina limehifadhiwa) iliyoko mtaa wa Mafisa manispaa ya
Morogoro.
Akisimulia mkasa huo, Meneja wa nyumba hiyo ya
kulala wageni jina tunalo alisema kuwa imekuwa ni desturi ya
askari huyo kwenda na vijana wa kiume katika nyumb
a hiyo hali iliyowatia wasisi wahudumu wa nyumba hiyo.
a hiyo hali iliyowatia wasisi wahudumu wa nyumba hiyo.
Alisema kuwa siku ya tukio askari magereza huyo
alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni majira ya saa 7.00 mchana akiwa
amempakia kijana mmoja katika pikipiki yake na kabla ya
kukabidhiwa funguo ya chumba namba 202, mhudumu wa nyumba hiyo alimwambia askari
magereza huyo kuwa masharti ya nyumba yao hayaruhusu watu wa jinsia mmoja kukaa
chumba kimoja.
Alisema kuwa askari huyo alimtambulisha kijana aliyekwenda
naye pale kuwa ni mdogo wake na kwamba walikuwa na mazungumzo naye ya muhimu na
baada ya mazungumzo hayo kijana huyo angeweza kuondoka.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya watu hao kuingia
chumbani mmoja wa wahudumu alipita karibu na mlango wa chumba
hicho na kusikia sauti ya mahaba, hali iliyomtiwa wasiwasi na kulazimika
kuripoti tukio hilo kwa meneja wake.
Majira ya saa 11.00 jioni askari huyo alitoka na
kijana huyo na kuahidi kurudi tena baadaye na aliporudi majira ya saa 1.00
usiku alirudi na kijana mwingine anayedaiwa kuwa mwenyeji wa
mkoa wa Tanga na kwa siku hiyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam baada ya
kupigiwa simu na askari huyo.
Askari huyo alingia chumbani akiwa na kijana huyo
na muda mfupi alitoka na kwenda dukani kununua kodomu na mafuta ya mgando
pasipokujua kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakifuatilia nyendo zake.
Aliporudi na kuingia chumbani baadhi ya vijana
waliokuwa wameandaliwa walizunguka nyuma ya chumba hicho na kuchungulia
dirishani na ndipo walipojionea mambo yote yaliyokuwa yakiendelea chumbani
humo.
Majira ya saa 2.00 usiku baada ya mambo hayo
kumalizika kijana huyo alitoka na kumuacha askari huyo akioga hata hivyo kabla
hajafika mbali meneja wa nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa na wakazi wengine
wa mtaa huo walionesha kukerwa na kitendo kile walimvamia kijana huyo wakitaka kumhoji
sababu za kushiriki kitendo kile cha aibu.
Hatahivyo, wakati wananchi hao chini ya mjumbe wa
seriakli ya mtaa wa Mafisa, Amina Mandawa, wakiendelea kumbana kijana huyo askari huyo
alifika katika eneo hilo akiwa na pikipiki yake na kujikuta akipokea kipigo
baada ya kubainika kuwa ndiye aliyekuwa akimlawiti mtoto huyo.
Kufuatia dhahama hiyo, askari polisi wanaotumia pikipiki
maarufu kama ‘Vodafasta’ alifika katika eneo hilo na kuwanusuru watu hao na
kibano cha wananchi na kufanikiwa kuwapeleka kituo kikuu cha polisi kwa
mahojiano.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile,
amekiri jeshi lake kumshikiria askari magereza pamoja na kijana anayedaiwa
kulawitiwa na askari huyo kwa muda kabla ya kuachiwa kwa dhamana siku hiyohiyo
majira ya saa 8.00 usiku.
Kamanda Shilogile alisema kuwa tayari jalada
limefunguliwa na kupelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kama ilivyo
utaratibu wa sasa ambapo kesi zote za jinai hazisimamiwi na jeshi hilo kama
ilivyokuwa awali.
Habari zaidi zinadai kuwa askari magereza huyo
amehamia mkoani Morogoro miezi minne iliyopita akitokea Arusha ambako nako
inadaiwa alihamishwa kutokana na kuwa na tabia ya kulawiti vijana wadogo.
IMENADLIWA NA:
Venance George, Hamida Shariff na Juma Mtanda,
Morogoro
0 comments:
Post a Comment