Kwa ufupi
Askofu Shoo aliyasema hayo jana alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu agizo liliotolewa na viongozi
wa dini jijini Dar es Salaam la kutaka mihadhara ya kidini izuiwe.http://www.mwananchi.co.tz
MOSHI.
ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Assembles of God mkoani Kilimanjaro, Glorious Shoo, amewataka wanasiasa kupima matamshi yao kabla ya kutamka hususan yanayohusu masuala ya udini ili kuepuka kuingiza nchi kwe
nye machafuko.
ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Assembles of God mkoani Kilimanjaro, Glorious Shoo, amewataka wanasiasa kupima matamshi yao kabla ya kutamka hususan yanayohusu masuala ya udini ili kuepuka kuingiza nchi kwe
nye machafuko.
Askofu Shoo aliyasema hayo jana alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu agizo liliotolewa na viongozi
wa dini jijini Dar es Salaam la kutaka mihadhara ya kidini izuiwe.
Alisema wanasiasa kila mmoja na chama chake ni
wakati wa kuhubiri amani na si kunyosheana kidole kwa sababu amani ya
nchi ikiondoka wote bila kujali chama, watakua vitani.
Shoo alisema kuzuia mihadhara ya kidini, hakumalizi tatizo na badala yake ni kuongeza tatizo .
Alisema kinachopaswa kufanyika ni Serikali
kawakamata wanaotumia mihadhara ya kidini, kukashfu dini nyingine.
Alisema tatizo la udini nchini sio kubwa na kwamba tatizo kubwa ni kuendelea kuwafumbia macho wanaotukana na kukashfu dini nyingine.
Alisema tatizo la udini nchini sio kubwa na kwamba tatizo kubwa ni kuendelea kuwafumbia macho wanaotukana na kukashfu dini nyingine.
“Vita ya ukabila ina mipaka, vita ya chama ina
mipaka, lakini vita ya udini haina mipaka maana hata kwenye nyumba ya
kupanga wako watu wa dini tofauti.
Ndugu zangu Watanzania tusithubutu kunyoosheana vidole kwenye udini jambo hili ni baya na hatari kuliko bomu,”alisema askofu Shoo.
Ndugu zangu Watanzania tusithubutu kunyoosheana vidole kwenye udini jambo hili ni baya na hatari kuliko bomu,”alisema askofu Shoo.
Aidha aliwataka viongozi wa dini kuwa na utamaduni
wa kukutana na kujadiliana kuhusu matatizo yao ikiwa ni pamoja na
kuwaonya waumini wanaochochea vurugu na kutoa maneno ya uchochezi dhidi
ya dini nyingine.
Askofu Shoo pia aliwataka waandishi wa habari kulinda amani ya nchi kwa kutoandika habari za uchochezi au kuegemea upande mmoja.
Alisema waandishi wa habari wananafasi kubwa ya
kueleza umma umuhimu wa amani iliyopo nchini na kuwaeleza pia madhara ya
vita wakitolea mfano vita vilivyoko kwenye nchi nyingine barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment