BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KATIBU CCM TAIFA KINANA KUMTAKA MBUNGE CHADEMA PETER MSIGWA AMUOMBE RADHI HADHARI, YEYE AMTAKA KWENDA MAHAKAMANI KESHO.


MBUNGE  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amewataka  wafanyabiashara  ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa  kuendelea  kufanya kazi katika  eneo la Mashine  tatu  bila  kufanya  vurugu  zozote kwa  wale wanaozuia kufanya  hivyo.
Akizungumzia  suala la Machinga  kuendelea  kunyanyasika  mbunge Msigwa amesema  kuwa tayari suala  hilo ameanza  kulipigania bungeni  kwa waziri  mwenye dhamana  hivyo kamwe  machinga  Iringa  wasikubali  kunyanyasika .
Aidha mbunge  huyo amemtaka  katibu mkuu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Bw  Kinana  kutosubiri muda  wa  siku  21 alizozitoa  kumfikisha mahakamani kuwa  yupo tayari  kwenda mahakamani hata kesho. 
Mbunge Msigwa amesema kuwa katika  ukweli kama  hata  kuwa tayari kumwogopa mtu na kuwa siku  zote atasimama katika  ukweli katika  kupigania maslahi ya Taifa  hili. 
Mbunge  Msigwa amesema  kuwa hatua ya katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bil
a yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na kumwogopa na  hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani  si  sawa ni  kumtishia nyau mtu mzima. 
Kwani  alisema  kuwa  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote .
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi  wa  jimbo hilo jioni hii katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani
Umati mkubwa  wa  wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao wa  jimbo la Iringa mjini
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini
CHANZO: FRANCIS GODWIN
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: