Kwa ufupi
Dalili za kuibuka mjadala mkali katika bajeti
ya leo zilianza kujitokeza mwishoni mwa wiki wakati wa semina ya wabunge
kuhusu masuala ya gesi ambapo wizara hiyo ilibanwa juu ya mambo ya
mikataba.http://www.mwananchi.co.tz
Dodoma/Mtwara. Wakati mjadala mkali ukitarajiwa kuibuka bungeni
leo wakati Serikali itakapokuwa ikiwasilisha bajeti ya Wizara ya Nishati
na Madini, joto limezidi kupanda mkoani Mtwara ikielezwa kuwa wananchi
wamehamasishana kwa mara nyingine kuacha shughuli zote ili kusikiliza
kama hotuba hiyo italinda masilahi yao.
Hotuba hiyo ambayo itasomwa leo mara baada ya
kipindi cha maswali na majibu bungeni na Waziri wa wizara hiyo, Profesa
Sospeter Muhongo, inatar
ajiwa kuibua mengi yakiwamo yanayohusu suala la gesi ya Mtwara.
ajiwa kuibua mengi yakiwamo yanayohusu suala la gesi ya Mtwara.
Mjini Mtwara vipeperushi vinavyopingana
vilisambazwa kuhamasishana ‘kuacha shughuli zao zote na kubaki nyumbani
ili kufuatilia matangazo ya televisheni wakati Profesa Muhongo
atakapotangaza bajeti hiyo, huku vingine vikipinga.
Ahadi za matumaini
Licha ya kampeni hizo za watu wa Mtwara, Serikali
nayo imeweka matangazo katika vyombo vya habari likiwemo gazeti hili
ikieleza namna mikoa ya Mtwara na Lindi itakavyonufaika na utafutaji na
uendelezaji wa Gesi Asilia.
Tangazo lililotolewa na Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania limeainisha faida za gesi hiyo kwa Mkoa wa Mtwara
ukiwamo umeme utakaotokana na gesi asilia.
Pia imeelezwa jinsi mafunzo kwa vijana juu ya matatizo ya gesi asilia yaliyodhaminiwa na Wizara ya Nishati na Madini na kampuni mbalimbali kuanzia mwaka 2010.
Pia imeelezwa jinsi mafunzo kwa vijana juu ya matatizo ya gesi asilia yaliyodhaminiwa na Wizara ya Nishati na Madini na kampuni mbalimbali kuanzia mwaka 2010.
Vilevile imeelezwa jinsi uboreshaji wa huduma za
jamii kama ujenzi wa shule, hospitali na ujenzi wa viwanda kama kile cha
saruji cha Dangote na mitambo ya kusafishia gesi utakavyowanufaisha
wakazi wa mkoa huo.
Gesi hiyo ambayo pia inachimbwa katika Kisiwa cha
Songosongo inatajwa kwamba itawanufaisha wakazi wa Mkoa wa Lindi kwa
kupata umeme, kunufaika na kodi ya wawekezaji wa gesi na udhamini wa
mafunzo kutoka kampuni mbalimbali na wizara.
Wiki iliyopita Profesa Muhongo alijigamba kuwa
bajeti ya wizara yake atakayosoma leo itakuwa ya karne ya 22
itakayomaliza tatizo la umeme nchini kwa kuwa imetoa vipaumbele kwa
sekta binafsi kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Wabunge wapania.
0 comments:
Post a Comment