TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA
ASSALAM alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza
Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa
tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na
majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa
la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.
Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini.
Watanzania
kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili
ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la
Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na
inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika
wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote,
Wakristo na Watanzania wote.
Kwa
niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio
hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na
wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.
SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.
0 comments:
Post a Comment