BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DC RUNGWE KUCHUNGUZA MABASI YANAYOTOZA Sh1,000

Kwa ufupi
Mtu akipanda Kiwira kwenda Tukuyu ambapo ni kilometa 10 nauli yake ni Sh1,000 , akipanda KK ambapo ni kilometa tano kwenda Tukuyu.
TUKUYU. 
MKUU wa Wilaya ya Rungwe ,Crispin Meela ameahidi kufuatilia malalamiko ya wakazi wa wilaya hiyo juu ya kuwapo kwa daladala zinazotoza nauli ya Sh 1,000 kwa kila kituo kutoka Kiwira kwenda Tukuyu mjini.

Pia amewasihi wakazi wa wilaya hiyo kuripoti kero hiyo ofisini kwake mara moja wakiwa na namba za magari yanayofanya vituko hivyo ili kukomesha vitendo vya aina hiyo.


Mtu akipanda Kiwira kwenda Tukuyu ambapo ni kilometa 10 nauli yake ni Sh1,000 , akipanda KK amb

apo ni kilometa tano kwenda Tukuyu.

nauli yake ni hiyohiyo na hata wanaopanda mabasi Katumba ambapo ni kilometa mbili hadi Tukuyu nauli ni hiyohiyo hasa nyakati za asubuhi na jioni ’’ alisema Atupele Mwakyambiki wa Kitope.


Naye Yesaya Kilindu wa KK alisema nauli ya daladala hizo ni wizi mtupu na kwamba mabasi yanayoheshimu sheria ni yale yanayosafiri kati ya Mbeya hadi Tukuyu ama Kyela ambayo yanatoza Sh 500 tu. (Mwandishi Wetu)
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: