Kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Daniel amenusurika kifo baada ya
pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana uso kwa uso na gari.
Ajali hiyo
iliyoshuhudiwaeneo la Nunge Mkoani morogoro.Mashutuda wa tukio hilo
walipohojiwa na audifacejackson blog walidai kwambaharaka za dereva
huyo wa boda boda ndizo zilizosababisha ajali hiyo.
Mashuhuda wa ajali
hiyo wakielezea zaidi walisema mzee
mwenye gari iliyohusika katika ajali hii alikuwa akitokea Mji mpya na
alipofika kwenye makutano ya barabara alitoa ishara ya kukata kona
kuelekea upande wa mahakama ya mwanzo Nunge, ndipo boda boda huyo akiwa
na haraka zake katanua upande wa kushoto na kusombwa na gari kwa bahati
aliruka na kuiacha pikipiki”.
Askali wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Morogoro akishuhudia pikipiki hiyo ikiwa ndani ya uvungu wa gari hiyo,.
Uchunguzi
uliofanywa na audifacejackson blog umebaini kwamba Daniel ni
mfanyabiashara katika soko la Mji Mpya na kwamba bodaboda hiyo
aliikodisha na kwenda kufungasha bidhaa mjini huku akiwa hana leseni ya udereva.
Wananchi
wakiinyajua juu gari hiyo kwa lengo la kuitoa pikipiki hiyo,kufutia
tukio hilo gari hilo lilishindwa kutembea hadi pikipiki hiyo
ilipoondolewa
Wasamaria wema wakisaidi kunyajua gari ili kuitoa pikipiki iliyosababisha ajlai hiyo mkoani morogoro
Baadhi ya wananchi wakimshuhdia Daniel na kusniodwa kuamini kama kweli amepona kwenye tukio hilo
Dereva huyu wa boda boda alimchukua Daniel na kumpeleka nyumbani kwake kwani hakupata madhara makubwa kwenye tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment