Bingwa wa pool upande wa wanawake, Salame Eliud Mzumbe akipiga mahesabu ya kupiga kete kuingiza katika shimo wakati wa mashindano ya pool ya mkoa wa Morogoro ya Safari Lager Higher Lerning Pool Championship 2013 dhidi ya mpinzani wake, Jackline Sanga kutoka chuo cha uandishi wa habari (MSJ) katika mchezo uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijan
a Social hall Kiwanja cha Ndege Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Bingwa wa pool upande wa wanaume, George Tito kutoka Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akipiga mahesabu ya kupiga kete kuingiza katika shimo wakati wa mashindano ya pool ya mkoa wa Morogoro ya Safari Lager Higher Lerning Pool Championship 2013 dhidi ya mpinzani wake, Kiloya Kafuna wa chuo kikuu cha Mzumbe katika mchezo uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Social hall Kiwanja cha Ndege Morogoro ambapo alishinda kwa 3-2 katika mchezo wa fainali.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
CHUO kikuu cha Mzumbe kimetwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya mkoa wa Morogoro ya Safari Lager Higher Lerning Pool Championship 2013 baada ya kuitambia chuo cha Ardhi kwa ushindi wa bao 13-9 katika mchezo mkali wa fainali wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall Kiwanja cha Ndege mkoani Morogoro jana.
Akitangaza matokeo ya washindi katika mashindano hayo Mwenyekiti wa chama cha pool mkoa wa Morogoro, Patrick Legong’a alisema kuwa chuo kikuu cha Mzumbe ndiyo bingwa wa pool mkoa wa Morogoro baada ya kuilaza chuo cha Ardhi kwa bao 13-9 katika mchezo wa fainali.
Legong’a alisema kuwa Mzumbe ilitinga hatua ya fainali baada ya kuitandika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa idadi bao 13-7 wakati Ardhi yenyewe ikitinga hatua hiyo ya nusu fainali kwa kuizabua chuo cha Uandishi wa habari Morogoro (MSJ) kwa bao 13-10.
Alimtaja mshindi wa tatu kuwa ni chuo cha Uandishi wa habari Morogoro (MSJ) baada ya kukishinda Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa jumla ya bao 13-8.
Legong’a aliwataja washindi wa kwanza kwa mchezaji mmoja mmoja kuwa George Tito kutoka Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ndiye bingwa kwa upande wa wanaume baada ya kumshinda Kiloya Kafuna wa kikuu cha Mzumbe kwa bao 3-2 katika mchezo mkali wa fainali.
Salame Eliud kutoka chuo cha Mzumbe alitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake baada ya kujikusanyia pointi sita na bao nne wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Jackline Sanga kutoka chuo cha uandishi wa habari kwa kupata pointi aliyepata pointi nne wakati Lilian Simule kutoka Mzumbe aliambulia pointi mbili.
Mshindi wa kwanza kwa vyuo alijakulia kitita cha Sh500,000, mshindi wa pili sh 300,000 na mshindi tatu sh100,000 wakati mshindi wa kwanza kwa wanaume alikabidhiwa sh 150,000 huku mshindi wa pili sh100,000 wakati upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni sh100,000 na mshindi wa pili sh50,000.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya vyuo vinne ikiwemo Mzumbe, Ardhi, SUA na MSJ ikiwa na idadi ya washiriki 40.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment