BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CLOUDS MEDIA GROUP KUSAFIRISHA MWILI WA ALBERT MANGWEA KUTOKA AFRIKA YA KUSINI KUJA TANZANIA.

                                 Marehemu Albert Mangwea.
 
TAARIFA za Kampuni hiyo kusaidia zilianza kuenea tangu juzi, baada ya Kamati ya Mazishi kushindwa kutaja makampuni, taasisi na watu walioanza kuchangia kwenye msiba huo.Picture
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
 
"Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea,” alisema kwa ufupi. 
 
Ngwea amepangwa kuletwa Tanzania kesho Jumamosi na kuagwa Jumapili, kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake.
  Barua inayoonyesha walioanza kuchangia msiba wa Ngwea.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
 
KAMPUNI ya Clouds FM, imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa ajili ya kuutoa Afrika Kusini hadi Tanzania kwa ajili ya kuzikwa, ukiwa ni utaratibu unaoonyesha kuwa wadau wote wameamua kushirikiana katika suala hili.

Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, alithibitisha kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya nyota huyo wa Bongo Fleva.CHANZO: HANDENI KWETU
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: