Kwa ufupi
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu
wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema wamepata taarifa kuwa katika vikao
vya viongozi wa mikoa hiyo, wamekuwa wakiishutumu CUF kuwa ndiyo
inayosababisha vurugu hizo.
http://www.mwananchi.co.tzNaibu Katibu Mkuu
wa CUF, Julius Mtatiro
DAR ES SALAAM.
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekana kuhusika na vurugu zinazotokea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na kwamba zinatokana na sera mbaya za Serikali za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekana kuhusika na vurugu zinazotokea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na kwamba zinatokana na sera mbaya za Serikali za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa
CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema wamepata taarifa kuwa katika vikao
vya viongozi wa mikoa hiyo, wamekuwa wakiishutumu CUF kuwa ndiyo
inayosababisha vurugu hizo.
“CUF haiungi mkono vurugu, tunataka wananchi wadai
haki zao kwa njia ya amani lakini inapotokea wananchi wakafanya vurugu
Serikali iwajibike kwani yenyewe ndiyo imezuia haki za wananchi,”
alisema Mtatiro.
Alisema mfumo wa stakabadhi ghalani katika ununuzi
wa korosho na gesi ni mambo yanayowafanya wanan
chi wa mikoa hiyo kusababisha vurugu.
chi wa mikoa hiyo kusababisha vurugu.
Mtatiro alisema kwa mfano zao la korosho, wakulima
wamekuwa wakidhulumiwa kwa kutokulipwa fedha za awamu ya pili kwa
kisingizio cha kushuka kwa bei ya zao hilo katika soko la dunia.
“ Kilo moja ya korosho inauzwa kwa Sh1,200 kwa
mfumo wa stakabadhi ghalani, awamu ya kwanza hulipwa Sh600 lakini awamu
ya pili wamekuwa hawalipwi ama wakati mwingine wanalipwa Sh200,
zinazobaki Sh400 zinakwenda wapi, ndiyo maana wananchi hawa wanafanya
vurugu,” alisema.
Alisema wananchi wa Lindi na Mtwara wanafahamu haki zao na kuzidai.
“CUF inaionya Serikali ya CCM isitafute mahali pa
kubambikizia makosa, viongozi wa CUF wasiendelee kugeuzwa kuwa ndiyo wa
kuhojiwa kuhusu makosa ya Serikali na CCM,” alisema Mtatiro katika
taarifa yake.
Alisema Serikali inapaswa kuwahoji watendaji wake na sera zake mbovu, ilizoshindwa kuongoza nchi.
Kwa mujibu wa CUF, wabunge kadhaa wa Mikoa ya
Lindi na Mtwara walihojiwa katika vikao hivyo wakidaiwa kuwa ni miongoni
mwa watu wanaopandikiza chuki kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment