Kwa ufupi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert
Boaz alithibitisha kukamatwa kwa askari hao: “Mchakato wa kuwafikisha
mahakama ya kijeshi unaandaliwa. Bangi hiyo ilikuwa inapelekwa kwa
mfanyabiashara mmoja huko Rombo na ndiye aliyewakodi.”http://www.mwananchi.co.tzMkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema.
GARI aina ya Toyota Landcruiser linalotumiwa na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Arusha, lilikamatwa juzi mjini Moshi likiwa limesheheni magunia 18 ya bangi.
Habari za awali zilieleza kuwa gari hilo
lilikamatwa juzi saa 4:00 usiku katika Mji mdogo wa Himo, Moshi Vijijini
likisafirisha bangi hiyo kwenda Tarakea, Rombo.
Polisi wawili akiwamo dereva wa gari hilo wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Himo na gari lipo Makao Makuu ya FFU, Moshi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert
Boaz alithibitisha kukamatwa kwa aska
ri hao: “Mchakato wa kuwafikisha mahakama ya kijeshi unaandaliwa. Bangi hiyo ilikuwa inapelekwa kwa mfanyabiashara mmoja huko Rombo na ndiye aliyewakodi.”
ri hao: “Mchakato wa kuwafikisha mahakama ya kijeshi unaandaliwa. Bangi hiyo ilikuwa inapelekwa kwa mfanyabiashara mmoja huko Rombo na ndiye aliyewakodi.”
Hata hivyo, Kamanda Boaz alisema atatoa taarifa zaidi leo kwani uchunguzi bado unaendelea.
Bangi ilivyonaswa
Habari zimeeleza kuwa polisi waliokuwa doria
waliliona gari hilo likitengenezwa na waliamua kuwauliza wenzao
kulikoni? Wakajibiwa kuwa kuna kitu walikuwa wakirekebisha na lilikuwa
ni tatizo dogo tu.
“Walipoulizwa kwani mnaelekea wapi wakasema
wanapeleka mzigo wa bosi huko Tarakea mpakani na kwa taratibu zetu za
kijeshi huwezi kuuliza ni bosi gani,” kilidokeza chanzo kimoja ndani ya
polisi.
Hata hivyo, polisi hao wa doria walirudi katika
gari yao ili waendelee na doria lakini baadhi ya polisi wakamweleza
ofisa aliyekuwapo katika gari hilo kwamba wanashuku gari lile limebeba
bangi.
“Lilikuwa na harufu kali ya bangi na hilo ndilo
lililowafanya wale polisi kurudi tena kwa wenzao na kuwaambia wanataka
waone wamebeba nini ndipo wakakutana na magunia 18 ya bangi,” kilieleza
chanzo chetu.
Inadaiwa kuwa baada ya kukuta bangi hiyo, polisi
hao waliwasiliana na Mkuu wa Upelelezi (RCO), Mkoa wa Kilimanjaro,
Ramadhan Ng’anzi ambaye naye alimjulisha Kamanda Boaz.
Ilielezwa kuwa Kamanda Boaz aliagiza kuwekwa mahabusu kwa polisi hao katika Kituo cha Himo na gari hilo lipelekwe FFU, Moshi.
0 comments:
Post a Comment