Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
Na Mohammed Kuyunga
WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ndiye waziri namba moja hadi sasa kwa
kulivunja mbavu Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma kutokana na
vichekesho vyake wakati alipokuwa akijibu hoja za wabunge mbalimbali hivi
karibuni.
Magufuli
ambaye wengi humuita ‘Jembe’ kutokana na uchapa kazi wake, alikuwa akiwasilisha
bajeti ya wizara yake na kuomba kuidhinishiwa Shilingi Trilioni 1.22 kwa mwaka
wa fedha 2013/14.
Mheshimiwa
huyo alimudu kuwafanya waheshimiwa wacheke sana huku ujumbe ukifika tofauti na
mawaziri wengine waliopita ambao hotuba zao zinadaiwa kuwa zilijaa ushawishi wa
usingizi.
“Tunajenga
barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma kwenda Iringa, wale watani zangu wa
Iringa hawatakuwa na haja ya kujinyonga kwenye miti, sasa watak
uwa wakilala
barabarani tu.”
Wabunge
walivunjika mbavu kwa vicheko.
Watani zake alimaanisha Wahehe ambao inadaiwa
wanapokuwa na hasira wana tabia ya kujiua kwa kujinyonga (ni madai).
Kama
vile haitoshi, waziri huyo akijibu swali la Mbunge wa Same Mashariki,
Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kuhusu barabara inayopita kwenye Kiwanda cha
Tangawizi kupewa hadhi, pia alitumbukiza utani.
“Mheshimiwa
Anne Kilango yale uliyosema tunayafanyia kazi, kuhusu barabara inayopita
Kiwanda cha Tangawizi kupewa hadhi tumepokea, maana pia mheshimiwa rais alitupa
maagizo.
“Nimeamini
una akili sana ndiyo maana mtani wangu Malecela alitoka Dodoma na kwenda
milimani Same huko, kwa nini hakuja usukumani?”
Aidha,
waziri huyo akimjibu Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ambaye alitoa
ushauri kwa Wizara ya Ujenzi kupunguza idadi ya miradi na kukamilisha mmoja
baada ya mwingine ili wizara iweze kufanikiwa huku akilalamikia kutojengewa
barabara jimboni kwake, Magufuli aliwavunja mbavu tena wabunge:
“…ushauri
wako ni mzuri ndiyo maana wizara yangu imeamua kuacha kujenga barabara jimboni
kwako ili tukamilishe sehemu nyingine kwanza…”
Hata
hivyo, wakati wabunge wakivunjika mbavu, Magufuli alisema Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) haina ubaguzi na itajenga barabara hiyo iliyoko jimboni kwa
mbunge huyo.
Akimjibu
Mbunge wa Viti Maalum (CCM –Bunda), Ester Bulaya ambaye alisema kwamba
anamkubali waziri huyo kutokana na utendaji wake, Magufuli naye alisimama na
kusema:
“Hata
mimi namkubali Ester Bulaya...”
Aidha,
Magufuli aliwashangaa wabunge wa upinzani ambao walionesha kutaka kumpinga na
kuwaambia kuwa bosi wao, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alionesha
kumkubali na kuzimwagia sifa sera za CCM baada ya kukamilishiwa barabara
iliyoko jimboni kwake Hai, Kilimanjaro.
“Kama
kuna mtu anabisha ushahidi uko hapa aje nimuoneshe, mheshimiwa aliandika kwenye
mtandao (akautaja jina zima) kisha akasema kama mtu haamini akatoa flashi yenye
sauti aliyodai ni ya Mbowe.
VIDOKEZO
VINGINE:
Alimwambia
mbunge wa upinzani ana moyo wa CCM CCM, amekaa ki-CCMCCM.
Katika
kutekeleza uvunjaji wa nyumba zilizoingilia hifadhi ya barabara aliwahi kuvunja
ukuta wa nyumba ya baba yake mzazi.
UKO KWENYE HUBA AU UTUMWA WA MAPENZI?-2

0 comments:
Post a Comment