Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema hayo bungeni
jana, wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha
2013/2014.
Alisema
Serikali inakamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma
hiyo jijini humo.
Kwa
mujibu wa Dk Mwakyembe, Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO),
ndiyo itakayokamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwende
shaji wa huduma
hiyo, atakayetumia miundombinu ya reli iliyopo na vichwa vya treni na mabehewa
maalumu ya usafiri katika miji.
Dk
Mwakyembe alisema mwitikio wa wananchi kutumia huduma ya treni ya abiria,
umekuwa mkubwa ikilinganishwa na uwezo wa kutoa huduma yenyewe, hususan nyakati
za mahitaji makubwa ya usafiri.
Wingi
wa abiria Kwa sasa kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, treni hiyo ya jijini Dar es
Salaam, inabeba watu 14,000 kwa kila siku, sawa na zaidi ya daladala 467 zenye
uwezo wa kubeba abiria 30 kila siku.
“Kwa
upande wa Tazara, wastani wa idadi ya abiria wanaosafiri kwa treni kwa siku,
umefikia 9,000 baada ya kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa mengine saba na
kichwa kimoja cha treni na kuanza kutumika rasmi Mei 9, 2013.
“Aidha,
kwa upande wa TRL, wastani wa abiria wanaosafiri kwa siku ni 5,000,” aliongeza
Dk Mwakyembe akizungumzia usafiri huo ulioanza Oktoba mwaka jana, kati ya
Stesheni na Ubungo Maziwa na kati ya Tazara na Mwakanga.
Faida,
changamoto Alisema kuanzishwa kwa usafiri huo wa treni jijini Dar es Salaam,
kumesaidia kumepunguza idadi ya magari barabarani.
“Kuanza
kwa usafiri huu, kumeshawishi baadhi ya wananchi waliokuwa wanatumia magari
binafsi kuja katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kuanza kutumia usafiri wa
treni,” alisema Dk Mwakyembe.
Alizitaja
baadhi ya faida zingine zinazotokana na usafiri huo, kuwa ni kupungua kwa
matumizi ya mafuta, muda unaotumika barabarani na hivyo kusaidia wananchi
kufika kwa wakati katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Alisema
Wizara inaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizojitokeza,
zikiwamo za kutokuwa na mfumo thabiti wa kukusanya mapato, uchakavu wa
miundombinu na uhaba wa injini na mabehewa.
Kuhusu
kuongeza huduma za usafiri huo, alisema Wizara imeunda Kamati Maalumu chini ya
uenyekiti wa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, ili kuchambua,
kuainisha na kushauri mipango na mikakati ya kuboresha na kupanua usafiri huo.
Ruti
mpya “Pia Wizara inaangalia uwezekano wa kuanzisha huduma maalumu ya treni kati
ya Stesheni ya Dar es Salaam na Gongo la Mboto kwa ajili ya kuhudumia abiria
wanaopita kwenda Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere,” alisema
Dk Mwakyembe.
Kwa
upande wake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilishauri kuwa ili mradi
huo ufanye kazi kwa ufanisi na kuondokana na hasara, Serikali iharakishe
kununua angalau treni mbili za kisasa na maalumu kwa safari fupi, ambazo
gharama yake ni Sh bilioni 8 kila moja.

0 comments:
Post a Comment