Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la
PolisiArusha.
JESHI la Polisi
Mkoani hapa limemkamata mtu mmoja aitwaye Ally Rashid Salimu (23) Mwendesha
pikipiki za abiria maarufu kwa jina la “Boda Boda” mkazi wa kata ya Sombetini
jijini hapa akiwa na bunduki aina ya shortgun Mossberg yenye namba T292166
ikiwa na risasi sita.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake leo saa 5:30 asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kwamba,
tukio hilo lilitokea juzi tarehe 28.04.2013 muda wa saa 3:00 asubuhi katika
maeneo ya Shamsi yaliyopo jijini hapa.
Alisema siku ya
tukio dereva huyo wa pikipiki akiwa katika eneo hilo alik
uwa anaendesha pikipiki aina ya Skymark yenye namba za usajili T. 615 BZL huku akiwa amebeba begi lilionekana kutuna sana, ndipo askari waliokuwa doria katika eneo hilo walimtilia shaka na kisha kumfuatilia na kufanikiwa kumsimamisha.
uwa anaendesha pikipiki aina ya Skymark yenye namba za usajili T. 615 BZL huku akiwa amebeba begi lilionekana kutuna sana, ndipo askari waliokuwa doria katika eneo hilo walimtilia shaka na kisha kumfuatilia na kufanikiwa kumsimamisha.
“Mara baada ya
kumsimamisha askari hao walipekua begi hilo na kukuta silaha hiyo ikiwa na
risasi sita na kisha kumfikisha mtuhumiwa huyo katika kituo kikuu cha polisi
cha hapa Arusha mjini”. Alifafanua Kamanda Sabas.
Kamanda Sabas
alisema upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
pindi utakapokamilika.
Tukio hilo la
ukamataji wa bunduki hiyo limekuja wiki tatu tu baada ya jeshi hilo kukamata
bastola moja pamoja na risasi 41 kutoka kwa watuhumiwa waliokuwa wanahusishwa
na matukio ya kumjeruhi Sister Mary Shobana na kisha kumnyang’anya fedha
taslimu Tsh 30,000,000/= (Milioni thelathini) eneo la Notre Dame Njiro lililopo
jijini hapa, fedha ambazo alitoka kuchukua benki ya Exim tawi la Shoprite.
0 comments:
Post a Comment