MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (pichani) amechaguliwa kwenye
mchakato wa kumtafuta “kinara wa Benki wa Afrika” kwa mwaka 2013 unaoendeshwa
na African Banker Awards chini ya African Development Bank Group.
Kinara
wa Benki wa mwaka ni tuzo inayotolewa kwa Viongozi (CEO`s) wa sekta ya benki na
fedha barani Afrika ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye mashirika yao hivyo
kuleta maendeleo katika sekta fedha na uchumi katika nchi zao na Afrika nzima
kwa ujumla.
African
Banker Awards imechagua vinara watano wa sekta ya fedha Afrika kuingia katika
mchakato huo ambapo mmoja wao ndiyo atakayejitwalia tuzo hiyo.
Zaidi ya Dkt.
Charles Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye
mabano ni Segun Agbaje-GTB Bank(Nigeria), Aigboje Aig-Imoukhede-Access
Bank(Nigeria), Andrew All
ly-Africa Finance Corporation(Nigeria) na Jao
Figuerdo- Unico Bank.
Dkt. Kimei ni mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye
mchakato huu tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, na
ni mtanzania pekee kwenye kinyang`anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na
mabenki kutoka nchini Nigeria na Afrika ya Kusini.
Hii ni fahari kubwa kwa
taifa letu kwani Dkt. Charles Kimei ni mtanzania anayeongoza benki kubwa ya
Tanzania inayoendeshwa na watanzania wenyewe.
Dkt.
Kimei, ambaye ni mchumi mwenye stashahada ya uzamivu, amefanya kazi katika
sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania alikokuwa
Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kabla ya kujiunga na Benki ya CRDB mwaka 1998
kama Mkurugenzi Mtendaji. Akiwa Benki ya CRDB ameingoza kutoka Benki iliyokuwa
ikijiendesha kwa hasara hadi kuwa Benki inayoongoza nchini.
Chini
ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imeweza kupata mafanikio makubwa
ikiwemo kutoka kutengeneza faida ya Shilingi billion 2 mwaka 1998 mpaka kufikia
Shilingi billion 108 mwaka huu, kuongeza mtandao wake wa matawi kutoka matawi
16 hadi matawi 97 mwaka huu.
Katika kipindi hiki pia Benki ya CRDB imekuwa
kinara wa kuleta bidhaa bunifu kwenye soko ikiwemo kadi zenye nembo za
kimataifa za MasterCard na Visa, ATMs za kutolea na kuweka fedha, mashine
maalum za kulipa kwa kutumia kadi (POS), Mikopo maalum ya Microfinance na
Wajasiriamali pamoja na kushinda tuzo za kimataifa za Chapa Bora yaani SuperBrands
kwa miaka minne mfululizo (2010-2013) na tuzo ya benki bora itolewayo na
Euro-Money mwaka 2004.
Chini
ya uongozi wa Dkt. Kimei, Benki ya CRDB imekuwa benki ya kwanza ya kizalendo
kuvuka mipaka na kufungua kampuni tanzu katika nchi jirani ya Burundi hivyo
kufungua milango ya ukuaji wa mahusiano ya biashara kati ya nchi hizo mbili na
ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kuingia
kwa Dkt.Kimei kwenye mchakato huu wa kupata kiongozi bora wa Benki wa Afrika
kunakuja muda mfupi tu baada ya kuteuliwa kwake bila kupingwa kuwa Mwenyekiti
wa Chama cha Mabenki nchini Tanzania (TBA). Mwenyekiti wa Chama Cha Mabenki
huchaguliwa na benki zote wanachama wa TBA.
Tunamtakia
kila kheri Dkt.Charles Kimei na Benki ya CRDB katika kuipeperusha vyema bendera
ya Tanzania katika tuzo hiyo. Habari kutoka kwa Habari Mseto Blog.
0 comments:
Post a Comment