NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013.
Mhe Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika
mjadala huu muhimu sana.
Hapa Afrika
kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi
ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya
kupigiwa mfano.
Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda
leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao
walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika
mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory
Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa
katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duni
ani.
Lakini leo Sierra
Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe
kwa wenyewe.
Naomba
nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa
jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu
Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba,
1998. Alisema.
“Mr. Speaker, after three years of my presidency, I
can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by
saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God
has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace,
love, rejoicing and exciding generosity.
It is a country of people who love equality and
justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of
human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct
policies of national building.
Policies based on the principles of social
justice, peace, harmony and development for all.
A unity which is
extra sensitive to policies, statements behavior and actions which may sore
seeds discard hatred and suspicious among Tanzanians”
Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri.
Lakini
naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja
kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna
mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa
sababu nchi yetu ina nyufa.
Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi
kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na
kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na
vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na
yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.
NDUGU
KABWE Z. ZITTO
Asubuhi hapa
Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa
chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani
kuhusiana na masuala haya ya kidini.
Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF
kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa
mpaka sasa chama cha wakristo.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa wenzetu
nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao
walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono
kupinga.
Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo
hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana
katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme
kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi
kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka
kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua
watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo.
Jana limetokea
tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja
watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana
wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na
ndio anachokitaka adui.
Ni hicho. Atakuja, wanaitwa “Agent
Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi
ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi
pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia
wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua
wakristo.
Wakati wa
tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu,
wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano
gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii.
Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja.
Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi
viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu wetu na
ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?
Mheshimiwa
Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge
utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila kujali
dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema.
Nimesikia hapa watu
wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo,
ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka
na bomu. Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu kama wananchi.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na
kauli za chuki “hate speeches”.
Kama hatuna vipengele vya kisheria
tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika hii
nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa
mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu
sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati
Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka
kuzungumza na waislam inafanya nini?
Inaenda
kuwaita BAKWATA.
Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres
masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT
ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji
wa shughuli za kidini.
Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba
tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si
ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi
au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya
Muungano wa Tanzania.
Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa
Mwenyekiti, nakushuru sana asante.
0 comments:
Post a Comment