Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani
(KNEC) Paul Wasanga.
BAADA YA KUJIBADILISHA |
BAADA YA KUJIBADILISHA |
MWANAUME
aliyegeuza jinsia yake, amelishtaki baraza la mitihani nchini, Kenya
National Examination Council (KNEC), akitaka lishurutishwe kubadilisha
vyeti vyake kuonyesha kwamba ni mwanamke.
Bi
Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla
ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato
cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001,
na amekuwa akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama
mwanaume katika vyeti vyake.
“Nimejaribu kuomba KNEC mara nyingi ibadilishe jina langu katika
cheti changu vya mtihani wa KCSE ili kionyeshe jinsia yangu halisi bila
kufaulu,” Bi Audrey aliambia mahakama.
Alisema hatua ya KNEC kukataa kufanya mabadiliko hayo, imemsababishia
mateso mengi kwa kubaguliwa na kunyimwa kazi.
Mahakama ilimruhusu
kuwasilisha ombi la kutaka baraza hilo liagizwe kutekeleza majukumu yake
kwa kurekebisha jina lake liwe na mwanamke.
Siku 14.
Anataka pia baraza hilo iagizwe kubadilisha alama inayoonyesha jinsia
yake inayoonyesha ni mwanaume katika cheti hicho na badala yake
ionyeshe kuwa ni mwanamke.
Mahakama ilipatia KNEC na Mkuu wa sheria muda wa siku 14 kujibu ombi la Bi Audrey.
Kesi itatajwa Mei 28 ili mahakama itoe maagizo zaidi.
0 comments:
Post a Comment