BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSAMVU TERMINAL FC YAJITULIZA KWA COMPOSSION LIGI DARAJA LA NNE TAIFA MANISPAA YA MOROGORO.

Mlinzi wa timu ya Compossion chini ya umri miaka 20 Jofrey Jofrey kushoto akimiliki mpira huku akizongwa na mshambulia wa Msamvu Terminal FC wakati wa ligi daraja la nne Manispaa ya Morogoro katika michezo inayoendelea kwenye uwanja wa Sabasaba ambapo mchezo huo Msavu Term
ila ilishinda kwa bao 3-2.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya Msamvu Terminal SC imeitandika timu ya Composion chini ya umri wa miaka 20 katika ligi daraja la nne inayoendelea katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro kwa bao 3-2.

Kabla ya ushindi huo kwa Msamvu Terminal SC ilipokea kipigo kikali kutoka kwa wafanyabiashara wa soko la matunda timu ya Mawenzi Market FC kwa bao 4-0 ambayo kwa sasa inaongoza ligi hiyo kwa pointi 13.

Vijana wa Composion ndiyo walioanza kupata mabao ya mapema yaliyopachikwa wavuni na Kassim Kassim dakika ya tano kwa bao la kwanza wakati bao la pili lilipatikana dakika ya tisa lililowekwa kimiani na mshambuliaji, John Chilunda kwa kujaza mpira wavuni kwa kichwa baada ya kupokea krosi iliyoelekezwa katika lango la Msamvu Terminal SC na kwenda mapumziko Composion ikiongoza kwa bao 2-0.

Kipindi cha pili Msamvu walitulia na kutandaza soka safi la kuonana chini ya kiungo mshambulia Mwaropanga Andendekisye na katika dakika ya 57 walifanya shambulizi langoni mwa wapinzani wao na kupata bao la kwanza lililopachikwa wavuni kwa kichwa na Hamza Lindu.

Katika dakika 67 kiungo huyo wa Msamvu Terminal, Mwaropanga Andendekisye aiisawazishia timu yake kwa bao la pili alilofungwa kwa kichwa huku bao la ushindi likitumbukizwa nyavuni na mshambuliaji Kalangula Boaz kwa kichwa na kufanya mchezo huo umalizike kwa Msamvu Terminal kuibukia na ushindi wa bao 3-2 ambapo ushindi huo umewafanya kufikisha pointi 12.
 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: