Mmoja wa vijana waliodaiwa kuwa mashoga akikata mauno.
PATI
ya Miss Utalii 2004 ambaye ni mwigizaji wa filamu za Kibongo, Sara
Mwakapala aliyomuandalia mwanaye Anthonio kumpongeza kwa kutimiza umri
wa miaka mitatu, nusu itibuke baada ya jamaa waliodaiwa ni mashoga
kufurika.
Katika
pati hiyo iliyofanyika maeneo ya Leaders, Kinondoni, Dar mwishoni mwa
wiki iliyopita, mbali na mashoga hao waliokuwa wakiserebuka taarab, pati
hiyo pia ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali ambao walimtuza Anthonio
fedha na zawadi kibao.
Akipiga
stori na Risasi Mchanganyiko, Sara alifunguka kuwa alifurahishwa na
tukio hilo la mwanaye kutimiza umri huo kwani malezi si mchezo,
yanahitaji kujipanga.
Sarah
alimzawadia mwanaye simu aina ya Ferrari yenye thamani ya Sh. laki tano
huku maandalizi yote ya shughuli hiyo yakigharimu Sh. milioni 3.
Wageni
waliomtuza mtoto huyo ni pamoja na Faiza ambaye ni mzazi mwenza wa
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na muuza nyago kwenye
video za wasanii wa Bongo Fleva, Mimah Mohamed ‘Baby Candy’.
0 comments:
Post a Comment