Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,
akimsikiliza, Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,
Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyelazwa Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini
Zanzibar baada ya kumwagiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikana huko maeneo
ya Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea
nyumbani kwake. Sheha huyo anaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali
ya Mnazi mmoja (wa pili kulia) ni Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed
Shein,akimuangalia Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi
Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) jinsi alivyoathirika na Tindikali
aliyomwagiwa na Mtu asiyejuilikanwa huko Tomondo juzi wakati alipokuwa
akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake, wakati Rais
alipomtembelea kumjulia hali Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi
mmoja .Kushoto Dkt.Slim Mohamed Mgeni. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
0 comments:
Post a Comment