CHANZO http://ndimara.blogspot.com
MOJA ya bango lenye ujumbe "Gesi ibaki au tugawane nchi" picha hii ni ya maktaba iliyopiwa katika vurugu hivi karibuni juu ya upingaji wa gesi kutoka Msimbati kwenda Dar es Salaam.
KILIKICHOPO MTWAARA SIYO MAASI.
WANANCHI na wakazi wa Mtwara wanaasi nini
na nani? Kilichopo Mtwata ni vuguvugu la wananchi kuwaambia watawala
kuwa kinachofanyika sicho.
Tena wanafanya hivyo kwa kuwakilisha wananchi
wengine pote nchini ambako mazingira kama yanayoonekana Mtwara yameleta
dhiki kuu kwa wengi na hata vifo.
Kumwaga askari polisi mjini Mtwara na mkoa mzima;
kuwaongezea askari wa Jeshi la Wananchi (JW); kufunika wananchi kwa
mabomu ya machozi, kufyatua risasi za moto, kuua mama mjamzito kwa
risasi moto; kujeruhi, kukamata wananchi kutoka majumbani mwao na
kuwalundika mahabusi - yote haya hayawezi kuwa suluhisho. Wala siyo
majibu kwa vuguvugu. Hapana !
Imefikia wakati vuguvugu linaanza
kuleta fafanuzi kali na kakamavu. Kwenye mitandao mko
noni, na hapa
naripoti, kuna kirefu cha Mtwara kama kinavyosambazwa:
M - Maarifa
T - Tunayo
W - Wazawa
A - Amkeni
R - Rais
A - Ametusahau
Nani ameandika au nani amewaandikia? Ubunifu huu hauwezi kupuuzwa au
kudharauliwa. Hauwezi pia kuzimwa kwa mabomu ya machozi, kamatakamata na
hata mauaji ya raia. Yuko wapi mtu wa nje (ya nchi) anayechochea
wananchi kuandika haya?
Kilichoko Mtwara ni vuguvugu la kutoa
tahadhari kwa watawala, kwamba yaliyotokea kwingine nchini yasitokee
Mtwara.
Ni hivi:
Kila palipopatikana madini nchini, watu walihamishwa;
mali zao zilichukuliwa au kuharibiwa; wengine wanatajwa kufukiwa wakiwa
hai ndani ya "migodi" - mashimo waliyochimba kwa mikono. Ni vilio vya
miaka mingi. Jinsi machozi yanavyoendelea kuwatiririka; ndivyo dhahabu,
almasi, tanzanite na madini mengine yanavyozidi kutiririkia mikononi mwa
wanaoitwa wawekezaji. Hakika hawa ni wawekezwaji.
Itashangaza
kila mmoja mwenye akili timamu iwapo serikali itashindwa, itakataa,
itadharau kukaa chini na wananchi na kuwaambia; na hata kuwaeleza kwa
maandishi - kwamba kuna mikataba hii hapa - iwe wazi na kuonyeshwa kwa
wawakilishi wao bungeni; kuna mafao haya - na wao wajue watanufaikaje;
kuna sera au tupe maoni ya sera ya uchimbaji gesi - ndipo iendelee
kutekeleza miradi yake.
Kwani miardi hii ni ya nani na kwa
faida ya nani? Kama ni kwa faida ya wananchi na wananchi wanataka kujua
mafao yake kwao, kwanini wasiambiwe na hata kushirikishwa kikamilifu
katika kuweka vipaumbele vitakavyotumia mafao hayo ?.
Katika
baadhi ya nchi, serikali zimejipangia, kwa mfano: Mapato yote kutokana
na dhahabbu yatakwenda kwenye hudumia ya wajawazito na watoto. Mapato
yote kutoka almasi, yatakwenda kwenye elimu ya msingi (darasa la kwanza
hadi 14). Mapato yote kutoka tanzanite yatakwenda kuhudumia elimu ya
juu. Mapato yote kutoka gesi asilia yatakwenda (eneo jingine kwa manufaa
ya umma kwa ujumla).
Utawala nchini hauna mipango ya aina hii.
Mtasomewa tarakimu walizotaka kusoma na hutajua kipi kimetumika wapi na
kiasi gani. Na kama kuna usiri tangu mwanzo, bila kujua mikataba
inasemaje na mavuno yatakuwaje; basi kila mmoja anaona "sasa tumeliwa."
Dhabu iliyoibwa na kampuni ya Meremeta kwa ushirikiano na wanasiasa,
haitafahamika; bei waliyouzia haitatajwa. Walionufaika hao ndio
kitendawili. Ni vitu jumlajumla tu. Kiza.
Kitu kimoja
hakiwatembelei watawala akilini. Ni kwamba miongoni mwa askari
wanaokwenda kukamata, kupiga, kulipua mabomu na wakati mwingine kuua;
kuna watoto, ndugu na jamaa wa wazazi, ndugu na marafiki wa wanaodai
kupewa maelezo juu ya gesi na vipi watafaidika nayo. Matokeo yake ni
nini huko tuendako?
Lakini ni kweli serikali inahitaji msaada
wa mawazo kuhusu hili? Kama inauhitaji, kwanini haiutafuti? Ni huu hapa:
Wape wananchi taarifa wanazotaka. Washirikishe katika maamuzi.
Washirikishe katika kujenga miradi. Washirikishe katika kulinda miradi
hiyo. Tatizo liko wapi ?.
Serikali isikubali kufanya changamoto kuwa tatizo; linaweza kuishinda kulimaliza.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment