MWANANCHI.Shughuli za mauzo na manunuzi zilirejea rasmi jana mjini Mtwara, baada
ya huduma hizo kusimama kwa siku tatu kutokana na vurugu zilizotokea
kuanzia Alhamisi baada ya kusomwa hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini
na wana-Mtwara kubaini kuwa suala lao la gesi halijapewa umuhimu
unaostahili. Picha na Abdallah Bakari.
MTWARA.
MKUU wa vikosi vya aridhini wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali SM Kijuu amewahakikishia ulinzi wafanyabiashara hao, baada ya kukutana na uongozi wa Chama cha Wafanyabiashara Sokoni (Wabisoco) jana asubuhi, kufuatia wafanyabishara hao kudai kuendelea kusitisha biashara zao kwa kuhofia usalama.

Katibu wa Wabisoco, Saidi Namata ameliambia
Mwananchi Jumapili kuwa wafanyabiashara hao wamekubaliana kufungua
biashara zao, baada ya makubaliano ya kulinda eneo hilo na askari wa
JWTZ.
“Sisi wafanyabiashara tulikuwa tayari kuendelea
kusitisha huduma kutokana na hali ya usalama kuwa mbaya, alipokuja
kiongozi wa jeshi na kutuhakikishia kuwa dhamana ya ulinzi itakuwa chini
yao tulikubaliana,” alisema Namata.
Alisisitiza: “Kama ulinzi ungekuwa mikononi mwa
polisi, katu tusingefungua.
Polisi wenyewe ndiyo hawa wanaovunja maduka na kuiba, kwa kuwa dhamana hii imebebwa na wanajeshi hatuna shaka, tunaomba wafanyabiashara wengine wafung
ue biashara zao.”
Polisi wenyewe ndiyo hawa wanaovunja maduka na kuiba, kwa kuwa dhamana hii imebebwa na wanajeshi hatuna shaka, tunaomba wafanyabiashara wengine wafung
ue biashara zao.”
Tangu juzi magari ya matangazo yamekuwa yakipita
mjini Mtwara na kuwatangazia wananchi kuendelea na kazi zao kama kawaida
kwa kuwa ulinzi umeimarika, huku askari wa JKT na JWTZ waliosheheni
silaha wakizunguka mitaani.
Pinda awasili Mtwara
Wakati tukiewnda mitamboni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewasili Mtwara jana jioni na kukutana na viongozi wa mkoa.
Bungeni Dodoma
Suala la mgawanyo wa rasilimali za taifa jana
liliendelea kutikisa Bunge, baada ya baadhi yao kueleza kuwa ni haki kwa
maeneo yanakotoka rasilimali hizo kunufaika kwanza kabla ya maeneo
mengine.
Wakati wabunge hao wakieleza hayo, wengine
wamesisitiza kuwa kwa kuwa nchi ni moja Tanzania, rasilimali zote ni
mali ya Watanzania wote.
Wabunge wanaotaka rasilimali zinufaishe kwanza
maeneo zinakotoka.
Wanasema pamoja na ukweli kwamba Tanzania ni moja, watu hao wana haki ya msingi kupata huduma hizo kwanza kuliko wengine.
Wanasema pamoja na ukweli kwamba Tanzania ni moja, watu hao wana haki ya msingi kupata huduma hizo kwanza kuliko wengine.
Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige alisema
anashangaa kwa nini fomula ya rasilimali kuyaendeleza maeneo
iliyopatikana, inatumika kwenye Idara ya Wanyamapori na haitumiki katika
sekta ya nishati na madini.
0 comments:
Post a Comment