www.mwananchi.co.tzMbunge wa Simanjiro Chrisptopher Ole- Sendeka, akionyesha ripoti ya
Mkaguzi Ernest&Young kuhusu Shirika la Umeme nchini na kudanganywa
kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kulik
ofanywa na
watendaji wake, wakati wa uchangiaji wa mjadala wa Nishati na Madini,
bungeni Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman.
BAJETI ya Wizara ya Nishati na Madini imepita kwa mbinde, huku
Bunge likiunda kamati maalumu kuchunguza chanzo cha mgororo wa gesi
mkoani Mtwara.
Bajeti hiyo imepita baada ya Waziri Profesa
Sospeter Muhongo kufanikiwa kuzima kusudio la wabunge saba waliotaka
kuikwamisha kwa kuondoa shilingi kama hoja zao hazijapata majibu ya
kuridhisha.
Wabunge waliotishia kuondoa shilingi kwenye bajeti
hiyo ni John Mnyika (Ubungo), Ezekiah Maige (Msalala), Christopher Ole
Sendeka (Simanjiro), Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini) James Lembeli
(Kahama), Dk Khamis Kigwangalla (Nzega) na Tundu Lissu (Singida
Mashariki).
Wabunge hao walitaka kuikwamisha bajeti hiyo kutokana na hoja mbalimbali,huku wengi wao wakitaka majibu ya miradi ya utekelezaji wa mradi wa Rea kwenye majimbo hayo.
Waziri Muhongo akisaidiana na manaibu wake, George
Simbachawene na Steven Masele walifanikiwa kupangua hoja za wabunge hao
kwa kueleza mipango ya wizara katika kutekeleza madai yao na kuifanya
bajeti hiyo ikose upinzani.
0 comments:
Post a Comment