Katibu wa jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.Sheikh
Ponda Issa Ponda, akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba
cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi
Novemba 1, 2012.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi uchochezi, uvamizi wa kiwanja cha Markaz mali ya Agritanza Limited na wizi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 59.
Hukumu hiyo iliyoahirishwa kwa mara ya kwanza Aprili 18 mwaka huu itatolewa leo na Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa anayesikiliza kesi hiyo tangu walipofikishwa mahakamani Oktoba 18 mwaka jana.
Oktoba 18 mwaka jana, Ponda na wenzake walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza wakikabiliwa na makosa ya kula njama kinyume na kifu
ngu 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012.
Wanadaiwa kwamba Oktoba 12 mwaka huu, eneo la Chang’ombe Markaz washitakiwa wote walikula kwa nia ya kutenda kosa hilo.
Katika shitaka la pili wanadaiwa, bila kuwa na sababu za msingi washitakiwa hao waliingia kwenye kiwanja kinachomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha kiwanja hicho isivyo halali.
Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai washtakiwa walijimilikisha kiwanja kwa nguvu kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu. Pia wanadaiwa kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh 59,650,000 mali ya Kampuni ya Agritanza Ltd.
Shtaka la tano linamkabili Sheikh Ponda na Salehe Mukadam ambao wanadaiwa kushawishi Waislamu kwenda kuvamia na kujimilikisha uwanja wa Markaz, mali ya Agritanza Ltd.
Washtakiwa hao wawili wanasota rumande kwa kipindi chote hicho kwa sababu dhamana zao zilizuiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya usalama wao.
Aprili 3 na 4 mwaka huu, mawakili wa upande wa Jamhuri,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor na Yahaya Njama waliwasilisha majumuisho ya mwisho mahakamani hapo kwa ajili ya kuisaidia mahakama kufikia uamuzi ulio sahihi.
Upande wa Jamhuri uliomba washtakiwa watiwe hatiani na kupewa adhabu kwa mujibu wa sheria kwa vile waliweza kuthibitisha mashtaka bila kuacha shaka.
Upande wa utetezi uliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na iwaachie huru.
Ulidai kwamba washitakiwa hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.
CHANZO http://www.mtanzania.co.tz
0 comments:
Post a Comment