Ngwea amefariki dunia leo asubuhi katika moja ya vitongoji vya jiji la Johannesburg na baadaye wenzake walimkimbiza katika Hospitali ya St Helen Joseph.
HII NDIYO HOSPITALI AMBAYO MWILI WA MANGWEA UMEHIFADHIWA..
“Baada ya kufika tuliambiwa ameshakufa, lakini imetushangaza sana,” alisema mmoja wa marafiki zake.
Lakini rafiki yake mwingine ambaye alikuwa mwenyeji wake, alisema Ngwea alikuwa katika hali nzuri tu.
“Alikuwa aondoke leo kurejea nyumbani Tanzania, hivyo niliondoka nyumbani na kumuacha akiwa amelala. Lakini nikiwa njiani nilipigiwa simu kwamba alikuwa hajaamka na walikuwa wanampeleka hospitali.
“Baadaye walinipigia simu kwamba alipoteza maisha tayari. Nilishangazwa sana, hadi sasa sijajua kwa kuwa cheti chenyewe kimeandikwa kizungu lakini unajua mwandiko wa madaktari,” alisema rafiki yake mwingine.
Lakini inaelezwa, Ngwea alirejea nyumbani akiwa anaonekana mchovu na kusema anataka kupumzika. Siku iliyofuata alichelewa kuamka, hali ambayo iliwashtua wenzake baadaye kabisa.
Hospitali ya St Helen Joseph aliyolazwa iko katika barabara ya 1 Peth, Auckland Park jijini Johannesburg.
Ni moja ya
hospitali kubwa lakini inayotibu watu mbalimbali wakiwemo wa kawaida, kwa
nyumbani unaweza kuilinganisha na
Muhimbili.
1 comments:
Kweli maisha mafupi lakini muda mwingine 2nayafupiosha wenyewe
madawa ya kulevya ndio chachu cha vifo ving vya wasanii wasanii wetu bongo.
Post a Comment