HII NI SEHEMU YA BARUA
HIYO:
"Nakuandikia kwa maagizo niliyopewa na
mteja wangu, Ndugu Abdulrahman Kinana, kufuatia matamshi yako ya uwongo ambayo
yamemkashifu, kumfedhehesha na kumshushia hadhi, Matamshi hayo uliyoyatoa
mchana wa tarehe 21 April, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa
uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilaya ya Nyam
agana,
jijini Mwanza.
Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi.
Pamoja na watu hao walikuwepo pia waandishi wa habari, wakiwepo wanahabari wa magazeti,
radio televisioni. Habari zenye Maneno yako ya Kashfa zimeenea nchi nzima na
duniani kote kwa njia ya habari elektoniki, ikiwepo mitandao ya kijamii.
Habari hizo zinaendelea kusomwa hadi sasa, na
zitabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu katika intaneti na kwenye hifadhi nyingine
za habari"
"Katika Mkutano huo, ulisikika
ukisema maneno mengi ya Kashfa kwa mteja wangu, yakiwemo haya yafuatayo: Kinana
(na naomba waandishi w habari mnisikie na nyie usalama wa Taifa mkapeleke
habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia watanzania waiamini
ccm.
Kinana mikono yake si misafi hata kwenye
NASACO, Shirika la Meli Tanzania, kuna harufu ya ufisadi ndani yake, ajibu
hapa... Kinana Meli zake ndio zinahusika kubeba mapembe nchi hii, hajajibu hoja
hizo! kwa siku katika nchi hii tembo sitini na saba wanauwawa...
Hao ndio wanaokifadhili Chama cha Mapinduzi
wakina Kinana halafu wanakuja eti kuwashawishi watanzania muwasikilize na
kwamba Chama cha Mapinduzi eti ni kizuri.
Halafu leo tukikaa ndani ya Bunge
tunapojaribu kuwatetea wananchi tumeacha majimbo yetu, Haya mambo ninayaongea
ni hatari kwa sababu haya yote ni majangiri ni organized crime ni mtandao wa
kimataifa uko duniani kote. unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama
tunawatetea.."
Katika barua hiyo, mwanasheria
huyo amemtaka Msigwa amuombe msamaha yaishe au la atamvuruta mahakamani,
tena kwa vitisho .Nainukuu para ya mwisho :
"Nakuangaliza na kukutahadharisha kwamba
iwapo hutatimiza matakwa ya Mteja wangu kama yalivyoainishwa kwenye barua hii,
basi kesi itakayokuja dhidi yako itakuwa na madai makubwa na mengi kuliko yale
yaliyotajwa humu, na unaweza kubebeshwa mzigo wa uharibifu, hasara na madhara
uliyomsababishia Mteja wangu, pamoja na gharama za kesi nzima, ambazo zote
zinaweza kufikia mamilioni ya Shilingi za Kitanzania"
Kuna para kumi na mbili za barua
hiyo ambazo zinapatikanaukurasa wa 25 wa gazeti la mwananchi.
0 comments:
Post a Comment