LADY JAYDEE.
WAKATI Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura, Lady JayDee akitarajia kupanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani kujibu mashtaka yake dhidi ya Wakurugenzi wa Clouds Media Group, Mwanadada huyo ajipanga kukimbilia nje ya nchi.
Lady Jaydee ameanza kuchanganyikiwa kufuatia kesi hiyo kiasi cha kutamani kukimbilia nchi jirani ya Kenya ama Malawi ili kukwepa mkono wa sheria ama kuondoka machoni mwa maadui zake hao.
Akiandika katika ukurasa wa Tweeter Lad Jaydee alisema kwamba, "Kuna muda pesa tu ndiyo inaongea sijui nihamie Kenya nikaombe uraia huko ?
Au Malawi labda, mtanifuata?..."alisema Lady Jaydee katika ukurasa wake.
Kitendo cha Lady Jaydee kutamani kwenda kuomba uraia nje ya nchi inaleta hisia tofauti, kuzua maswali mengi yasiyo na majibu hasa baada ya kuzingatia kwamba hivi sasa uraia wa kununuliwa iko wazi katika nchi mbalimbali huku nchi kama ya Kenya ikizingatia umaarufu wa mwombaji kazi yake pamoja na kipato chake.
Endapo Lady Jaydee atatimiza ndoto yake ya kukimbilia nchi jirani za Malawi ama Kenya kwa lengo la kuinusuru roho yake pamoja mafanikio yake kimuziki, atakuwa msanii wa kwanza kukimbilia nchi jirani na pengine ikawa ni doa kubwa ambayo Serikali ya Tanzania inapaswa kufanyia uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha migogoro ya wasanii wa muziki na wamiliki wa vituo vya redio.
CHANZO http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment