WANAWAKE WA IRINGA WAKICHUNGA MBUZI.
WANANCHI wa Mkoa wa Iringa wamegundulika
kuwa wazito wa kuchangia shughuli za maendeleo kwa hiari na kusababisha
viongozi kutumia nguvu nyingi ili kufanikisha uweesshaji wa michango.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na asasi
isiyokuwa ya kiserikali ya Tuwafikie Tanzania umebainisha mapungufu 9
ambayo yanawahusu wananchi wa mkoa huo kwa kutowajibika ipasavyo katika
ujenzi wa maendeleo ya kijamii.
Bovan Mwakyambiki Mhamasishaji wa elimu
vijijini kupitia asasi hiyo ameluambia mtando huu kuwa maendeleo ya
kijamiii yanakwamishwa na jamii yenyewe kwa kutowajibika ipasavyo kwa
visingizio kadha wa kadha ambayo havina sababu za masingi.
Miongoni mwa sababu ya kutowajibika
imetajwa kuwa ni jamii kutokuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu
mbalimbali vya kijamii ili kupata taarifa zinazoweza kuwasaidia katika
maendeleo.
“Tumegundua kuwa watu wetu siyo wasomaji
wa vitabu na wazito kufuatilia taarifa zinazohusiana maeneo ya shughuli
zao. Haya ni pamoja na wafanyabiashara, wafanyakazi, wafugaji na
wakulima” amesema Bovan.
Amesema imekuwa ni desturi ya watu kutaka kila wanapoitwa kulipwa hata ama kuna shughuli ya kupata elimu bure.
“Wanapoitwa kwenye mafunzo huangalia
zaidi ni kiasi gani cha pesa watapata badala ya ni aina gani ya ujuzi
wanaotakiwa kuupata na kwa faida gani lakini hata hivyo tumegundua kuwa
sio wabunifu, wengi huishi maisha yaleyale, kwa mifumo ileile njia zile
zile” amesema.
Akifafanua zaidi Mwakyambiki amesema
wengi wao wana mitazamo hasi kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo hasa
linapoanzishwa jambo hata kama ni kwaajili ya jamii nzima na kufikiria
kuwa watu hubuni miradi ili wajinufaishe.
Kwa upande mwingine amesema hata viongozi
mbalimbali wa kiserikali wamekuwa wavivu kufikiri kwa kile
alichokieleza kuwa ni wapuuziaji wa mabo ya muhimu.
“Hupuuza historia ya mji na kuacha maeneo
ya kihistoria kuharibika bila kujali umuhimu wa kutunza na kuborehs
maeneo hayo, wengi hawapendi kujifunza na kutaka kujua hata kwa fursa
zinazojitokeza hawazizingatii. Huzipuuza kwa kujiona wanajua kila kitu”
amesema.
Amesema wananwake wa vijijini wanakumbwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutokuwa na uhuru wa kutoa mawazo
kwa kuwa bado wanakandamizwa na mfumo dume.
“Wanawake wa vijijini bado hawana uhuru
wa kutoa mawazo yao na kuelezea hisia zao kwa uwazi, wengi ni waoga hasa
wanapokuwa kwenye mikutano ya hadhara na sehemu za majadiliano”
amesema.
Hata hivyo alisema imeonekana vinana
wengi huanza kujihusisha na ngono katika umri mdogo hali inayosababisha
mmomonyoko wa maadili na matatizo mengi katika jamii.
“Vijana huanza kujihusisha na mahusiano
ya kimapenzi katika umri mdogo sana, na hali hii inazidi kuleta hofu ya
kuwa na vijana wengi wanaoweza kuangukia maambukizi ya magonjwa ya zinaa
na Ukimwi” amesema. Chanzo http://gustavchahe.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment