Kwa ufupi.
Kwa uamuzi huo, washtakiwa hao wanaweza kuomba
dhamana wakati kesi yao itakapotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Mei 13, mwaka huu.http://www.mwananchi.co.tz
Mkurugenzi wa Usalama wa
Chadema, Wilfred Lwakatare akionyesha alama ya vidole V mara baada ya
kufutiwa mashtaka ya ugaidi katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana.
Picha na Michael Jamson.
DRA ES SALAAM.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewafutia mashtaka matatu ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewafutia mashtaka matatu ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura.
Mashtaka yaliyofutwa ni ya pili, tatu na nne.
Shtaka la kwanza ambalo ni la kawaida la jinai limebaki. Yaliyofutwa ni
kupanga njama za utekaji nyara dhidi ya Dennis Msacky kinyume na Kifungu
cha 21 cha sheria inayopinga ugaidi. Shtaka la tatu ni walipanga na
kushiriki katika mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara
dhidi ya Msacky na la nne ni lilikuwa likimkabili Lwakatare la
kuhamasisha vitendo vya kigaidi.
Katika shtaka la kwanza ambalo ndilo lililobaki,
washtakiwa hao wanadaiwa kula njama kumdhuru Msacky kwa kutumia sumu
kinyume na Kifungu cha 227 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Kwa uamuzi huo, washtakiwa hao wanaweza kuomba dhamana wakati kesi yao itakapotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 13, mwaka huu.
Kwa uamuzi huo, washtakiwa hao wanaweza kuomba dhamana wakati kesi yao itakapotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 13, mwaka huu.
Katika uamuzi wake, Jaji Lawrence Kaduri wa
Mahakama Kuu alikubaliana na hoja za mawakili wa Lwakatare kuwa mashtaka
hayo hayana maelezo ya kutosha kuonyesha kuwa ni ya ugaidi akisema
yalipaswa yawe na maelezo yanayoelezea uhalisia wa ugaidi.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi
ya mawakili wa watuhumiwa hao kupinga uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka
(DPP) wa kuwafutia kesi na kis
ha kuwakamata na kuwafungulia tena kesi yenye mashtaka hayohayo kwenye Mahakama ya Kisutu, Machi 20, mwaka huu.
ha kuwakamata na kuwafungulia tena kesi yenye mashtaka hayohayo kwenye Mahakama ya Kisutu, Machi 20, mwaka huu.
Jaji Kaduri alikubaliana na hoja za Wakili wa
Serikali, Prudence Rweyongeza alizozitoa wakati wa usikilizwaji wa
maombi hayo kuwa uamuzi wa DPP ulikuwa sahihi.
Lwakatare na Rwezaura walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18 na kusomewa mashtaka hayo manne katika kesi namba 37 ya mwaka 2013.
Lwakatare na Rwezaura walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18 na kusomewa mashtaka hayo manne katika kesi namba 37 ya mwaka 2013.
Zombe aachiwa huru
Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane.

Hata hivyo, mahakama hiyo imetoa fursa nyingine kwa DPP kukata rufaa nje ya muda kwa kuzingatia Sheria ya Ukomo wa Muda.
DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu
iliyomwachia huru Zombe na wenzake katika kesi ya mauaji ya
wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva teksi mmoja
wa Manzese, Dar es Salaam.
Mahakama hiyo iliitupilia mbali kutokana na kasoro za kisheria zilizobainika katika taarifa ya kusudio la kukata rufaa.
Kasoro hiyo ni kuandika kuwa hukumu inayopingwa
ilitolewa na Jaji Salumu Massati wa Mahakama ya Rufani, badala Jaji wa
Mahakama Kuu.
0 comments:
Post a Comment