BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE ATUA ARUSHA KUTOA POLE KWA MAJERUHI WALIOLAZWA HOSPITALI YA MT MERU KUTOKANA NA MAJERAHA YA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA MT JOSEPH OLASITI ARUSHA.

 Mbunge wa arumeru mashariki-chadema Joshua Nasari(kushot)akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa arusha kwa ajili ya kuwapa  pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, 2013 Kulia kwake ni mbunge wa arusha mjini-Chadema Godbless Lema
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na watu mbalimbali muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa arusha kwa ajili ya kuwapa  pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe akiongea na waaandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Arusha kwa ajili ya kuwapa  pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013.kushoto kwak
e ni Mbunge wa Arumeru Mashariki-Chadema, Joshua Nasari na Kulia ni Kulia kwake ni mbunge wa Arusha mjini-Chadema Godbless Lema.Picha na Chadema

Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Mhe Freeman Mbowe jana jioni aliwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali ya Mt Meru kutokana na majeraha yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi, katika parokia teule ya Olasiti, Arusha, lililotokea Jumapili iliypoita, Mei 5, 2013.

Baadaye katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Mbowe aliwapa pole wote walioathirika kwa janga hilo kwa namna yoyote, na kuwataka Watanzania wote wawe watulivu wakati vyombo vya dola vinafanya kazi yake, lengo likiwa ni kuwapata wahusika ili ijulikane hasa lengo lao. 

Baada ya kutoka hopsitalini, Mbowe na msafara wake walielekea Elerai kuhani msiba mmoja wa waliofariki.

Mbowe katika msafara wake aliambatana na wabunge wa chama hicho kwa majimbo ya Arusha Mjini na Arumeru Mashariki, pamoja na viongozi wa juu wa Chama wa Kanda ya Kaskazini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: