Karina Mohamed 'Natalia' akiwa katika hospitali ya Amana.
http://shiladeux.blogspot.com
MAAJABU zaidi yamebainika kuhusu kijana wa kiume, Karina
Mohamed ‘Natalia’, 20, aliyelazwa wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke.
Karina, alilazwa wodi ya wanawake
akidhaniwa ni mwanamke kwenye Hospitali ya Amana ambayo ina hadhi ya mkoa
kitabibu, Ilala, Dar es Salaam, kabla ya kugundulika akiwa chumba ch
a maiti
baada ya kufariki dunia.
MAAJABU YA KWANZA; SURA.
Tumebaini kuwa sura ya Karina, haina
tofauti yoyote na ya mwanamke.
Uwazi limepata ushahidi wa picha za
Karina, enzi za uhai wake na kujiridhisha kwamba sura ya kijana huyo ilikuwa na
sifa nyingi za kike kuliko za kiume.
KUPTIA picha ambazo
alipiga akiwa amevaa nguo za kubana, imebainika kuwa Karina ambaye ana asili ya
Kiarabu, alikuwa ameumbika kwa sifa nyingi za kike.
Consolata Temu, 26,
aliyemfahamu Karina enzi za uhai wake, alisema:“Niwe mkweli, yule jamaa
aliumbika kike kuliko wanawake wengi sana.
Mimi mwenyewe niliwahi kumwambia
kwamba ningeumbika kama yeye ningeringa sana.”
Akaongeza:
“Hipsi za
Karina ni za kike zaidi. Nimewahi kukaribiana naye na kufanikiwa kumshika, yule
jamaa alikuwa na mwili laini mpaka unaweza kujiuliza alikuwa anakula nini.
Maana ni mwanamke kabisa.”
MAAJABU YA
TATU; SAUTI
Imeelezwa kuwa Karina
alikuwa na sauti nyembamba kiasi kwamba kila aliyezungumza naye, aliamini ni
mwanamke mpaka yeye mwenyewe alipoamua kueleza.
“Akinyamaza utaondoka
na imani kwamba umekutana na mwanamke. Wanaume wengi walimtongoza kwa kuamini
ni mwanamke. Ukizingatia ni mzuri sana.”
MAAJABU YA NNE; KIFUA
Imebainika kuwa
wauguzi kwenye Hospitali ya Amana, walishindwa kubaini kuwa Karina ni mwanaume
kwa sababu kifua chake, japo hakina matiti lakini kimekaa kama cha mwanamke.
Muuguzi mmoja
(jina tunalo), alisema: “Sisi tulijua maziwa yake ni madogo, maana alivyo
ni mwanamke mtupu. Tulishangaa sana kujua ni mwanaume, maana ni mzuri kuliko
hata sisi wengine hapa.”
MAAJABU YA TANO; TUMBO
Muunguzi huyo
alisema: “Kuna kipindi wakati wa kumhudumia, tulipandisha nguo na kumpima
tumbo. Sijawahi kuona tumbo la mwanaume likiwa laini vile. Lile ni tumbo la
kike. Huo ndiyo ukweli, kwa kweli hilo lilikuwa tukio la kwanza kuliona.
“Mtu mwenye sifa zote
za kike, baadaye kugundulika ni mwanaume, nilishangaa sana.”
MAAJABU YA
SITA; NYWELE
Kwa mujibu wa
muuguzi, Karina alifika hospitalini hapo akiwa na nywele ndefu ambazo
ziliwekewa dawa, kufanana kabisa na za mwanamke.
“Hakuna anayeweza
kutulaumu kabisa katika jambo hili. Hata angekuwa nani, asingekubali kama yule
ni mwanaume. Hata aliyegundua baadaye ni baada ya kumuona jinsia yake wakati
alipovuliwa nguo,” alisema.
Ukweli kuhusu nywele,
vilevile unajidhihirisha katika picha zake enzi za uhai wake, zinazomwonesha
akiwa ametengeneza nywele katika mitindo mbalimbali ya kike.
MAAJABU YA SABA;
NYETI
Rafiki wa Karina,
aliyeomba hifadhi ya jina lakei, alisema: “Yule jamaa alikuwa na ‘umbile’
dogo sana ambalo hakulifurahia. Kitendo cha kuwa na ‘umbile’ hilo, aliona
mkosi, ndiyo maana alikata tamaa, moja kwa moja akaamua kujishughulisha na
mapenzi ya kinyume na maumbile.
“Alijishughulisha na
vitendo vya ushoga na hili linafahamika kwetu sisi tuliokuwa watu wake wa
karibu na ndiyo maana alikuwa na vitendo vingi vya kike na alichukia kuitwa
mwanaume.”
KUZIKWA NA JIJI
Habari zinasema kuwa Karina ni raia wa Kenya, mwenye
asili ya Jiji la Mombasa, Uwazi limebaini kuwa mpaka sasa hakuna ndugu
aliyejitokeza kumtambua.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Dar es Salaam,
Marietha Minangi, alisema: “Hakuna ndugu aliyejitokeza, endapo zitapita siku
saba kabla ya ndugu kujitokeza, basi atazikwa na jiji. Siku saba zinahesabiwa
kuanzia pale alipofariki dunia.
0 comments:
Post a Comment