BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAALIM SEIF: TUKIO LA BOMU ARUSHA LISITUGAWANYE

hamad 370ee
Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar(SMZ),Seif Sharif Hamad ametamka ya kwamba tukio la shambulio la bomu lililorushwa katika kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi na kuua watu watano  huku 60 wakijeruhiwa lisitumike kama kigezo cha kuwagawa watanzania kwa misingi yao waliyojiwekea.

Makamu huyo wa kwanza alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea eneo la tukio hilo sanjari na kupata fursa ya kutoa mkono wa pole kwa majeruhi mbalimbali waliolazwa katika hospitali ya mkoa ya Mt Meru.

Alisema kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ila lisitumike kama njia ya kuwagawa watu kwa misingi yao ya dini na kabila.

Alisema kuwa kila mtu ana haki ya kuabudu dini yake bila kuvunja sheria wala kubugudhiwa kwa namna yoyote.
“Kila mtu ana haki ya kuabudu dini yake bila kuvunja sheria wala kubugudhiwa”alisema Hamad.

Hatahivyo,alitoa wito kwa watu wenye taarifa mbalimbali kushirikiana na vyombo vya ulinzi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana  kwa watuhumiwa.

Aliwataka wafuasi wa dini mbalimbali sanjari na wanasiasa nchini kutotumia mwanya wa tukio hilo kuleta mgawanyiko ndani ya jamii.

Katika hatuia nyingine meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo alisema kuwa tukio hilo litaathiri sekta ya utalii kwa ujumla na uchumi wa mkoa wa Arusha sanjari na wa taifa kw aujumla.

Lyimo,alitoa kauli hiyo wakati uongozi wa jiji la Arusha wakiwemo madiwani wa vyama tofauti mara walipotembelea hospitali ya St Elizabeth kukabidhi misaada ya mablanketi pamoja na fedha ambazo hakuwa tayari kutaja ni kiasi gani.

Kwa upande wake naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau wa utalii watajitolea kiasi cha fedha kisaidie kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili hospitali ya St.Elizabeth kutokana na kupokea wagonjwa wengi kwa wakati mmoja waliotokana na kadhia ya bomu iliyotokea kwenye uzinduzi wa kanisa huko olasit Nyalandu Alisema.

Kuwa kesho watakabidhi msaada huu wa mablanket na madawa ili kukabiliana na changamoto hiyo na kuwa wamewataka madaktari kama wanaona kunauwezekano wa majeruhi kupelekwa nje kwa kufanyiwa uchunguzi wawe teyari kuwaambia ili wajiandae kuwapeleka huku ilikuweza kubaini kama vyuma vilivyo miilini mwao kama vitakuwa na madhara.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: