JUMLA ya watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
mkoani Arusha kwa kutuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu lililorushwa katika
eneo la Kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi katika parokia teule ya Olasiti siku ya
Jumapili, Mei 5, 2013 na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi weng
ine
zaidi ya 60.Ripota wa WAPO FM radio ilisema majina ya watuhumiwa hao yametajwa kuwa ni:-
1. Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa
Mrombo, Arusha)
2. Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa
Mrombo, Arusha)
3. George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa
Olasiti, Arusha)
4. Mohammed Suleiman Said (38, mkazi wa
Ilala, Dar es Salaam, aliyewafuata kwa gari binafsi washukiwa wa ugaidi kutoka
kiwanja cha ndege na kuwepeleka hadi hoteli ya Aquiline iliyopo Arusha)
5. Said Abdallah Said (28, mkazi wa Abu
Dhabi, Nchi za Falme za Kiarabu)
6. Abdelaziz Mubarak (30, Nchi za
Falme za Kiarabu)
7. Jassini Mbaraka (29 mkazi wa Bondeni,
Arusha)
8. Foud Ahmad (28, Nchi za Falme za
Kiarabu)
9. Said Mohsen (Najran, Saudi Arabia)
Hata hivyo himaya ya Imarati, Nchi za Falme za Kiarabu (UAE - United Arab Emirates) inasema maafisa wake wamekanusha kuhusu raia wake watatu kuhusika na mlipuko wa bomu la Olasiti, Arusha.
Abu Dhabi ni mji mkuu wa Imarati (UAE), ambazo zina imirati saba -- Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Fujairah, Ras al Kaimah, Ajman na Umm a Quwain.
Nchi jirani na
UAE ni Qatar, Saudi Arabia na Oman.
0 comments:
Post a Comment