JESHI
la Polisi Mkoa wa Kinondoni linamshikilia Ahmad Mohamed Sharif (38),
mfanyabiashara na mkazi wa Mwananyamala Msisiri ’A’ kwa tuhuma za
kuwaingilia kinyume cha maumbile wanafunzi wanne wa darasa la nne wa
Shule ya Msingi Misisiri ’A’.
Ahmad amekuwa
akiwaingilia kinyume cha maumbile wanafunzi hao katika kipindi cha
mwezi Aprili na Mei mwaka huu kwa nyakati tofauti.
Kati ya
wanafunzi hao, wawili wana umri wa miaka 10 na wengine wawili wana umri
wa miaka 12 na 11 wote wakiwa ni wanafunzi wa Misisiri A.Mwalimu Mkuu wa
shule hiyo, Suzana Orege (35) alisema wanafunzi hao wamekuwa na
mahudhurio mabaya shuleni kwa zaidi ya mwezi mmoja na ndipo walipojaribu
kuwafuatilia kwa karibu ili kubaini sababu za wanafunzi hao
kutohudhuria shuleni.
Suzan alisema ilipofika Mei 9, mwaka huu
walifanikiwa kuwapata wanafunzi watatu (majina yanahifadhiwa) lakini
mmoja alikimbia kusikojulikana na walipowahoji sababu za wao
kutohudhuria masomo, waliwaeleza kuwa huwa wanatoka nyumbani kama
kawaida kwa ajili ya kwenda shule, lakini huishia nyumbani kwa
Ahmed.
Alisema walipohojiwa zaidi walisema baada ya kufika nyumbani
kwake huwawekea CD za ngono na kisha kuwaingilia kinyume cha maumbile na
kuwapa maandazi, chapati, bagia, biskuti na kuwatishia wasiseme kwa mtu
yeyote na endapo watasema atawafanyia kitu kibaya sana. Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Charles
Kenyela amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, ambapo alisema
alikamatwa Mei 10, mwaka huu na atafikishwa mahakamani kesho.
Kamanda
ametoa onyo kwa watu wengine wenye tabia chafu kama hiyo kuacha mara
moja kabla ya kukumbwa na mkono wa sheria.
0 comments:
Post a Comment