Josephat maimu aliyejeruhiwa katika mateka yaliyofanywa na majambazi
katika poli la kanembwa akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya
kibondo hivi karibuni.
Kijana huyo Emilius Lukius (20), akizungumza na Mtanzania jana nyumbani kwao, alisema alitekwa na watu sita asiowafahamu saa tatu asubuhi maeneo jirani na nyumbani kwao, wakati akielekea kuchukua maziwa.
“Nilikuwa nimetumwa maziwa na shangazi, nikafuata maeneo ya jirani na hapa nyumbani, kabla sijafika nilikutana na gari dogo yenye rangi nyeupe, ikasimama wakas
huka watu sita, wakanibeba na kuniingiza ndani ya gari.
“Nilipofika ndani ya gari wakanifunga kamba mikononi, miguuni na mmoja aliniziba mdomo wakaanza kunipeleka walikokuwa wakielekea wao, sikuweza kufahamu ni maeneo gani tulifika isipokuwa kulikuwa na pori, wakanishusha na wenyewe wakashuka.
“Waliniacha chini wenyewe wakasogea mbele kidogo nikaona wanatoa mapanga na visu, nilipohangaika hangaika nikaona kamba ya mikononi imelegea, nikachomoa mikono, nikajifungua miguu kisha nikaanza kukimbia,’ ’alisema.
Alisema walipoona kakimbia walianza kumkimbiza, alifanikiwa kuwapotea baada ya kujificha katika kichaka, alikaa kichakani huku akitafuta namba za nyumbani kwao kwa ajili ya kupiga simu ili wamfuate alipokuwa.
“Nilimpigia shangazi simu, sikujua nilipokuwa, nilitoka kichakani na kutafuta mahali ambako wangeweza kuniona, nilishtuka niko baharini.
“Nilimuona Polisi mmoja, akaniuliza natafuta nini, nikamuelezea, akaniomba simu yangu, aliwasiliana na ndugu zangu kuwafahamisha nilipokuwa, alinipeleka ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa JKT Mbweni, shangazi yangu alinifuata huko na kunirudisha nyumbani,’’ alisema na kuongeza kwamba hajui walimteka kwa sababu gani.
Akizungumza na MTANZANIA kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema bado hajapata taarifa za tukio hilo.
“Sina taarifa za tukio hilo, kama amesharipoti kituo cha Polisi tutalishughulikia, wiki iliyopita tulifanya msako maeneo hayo na kuwakamata watu wengi, tutaendelea na msako,’’ alisema Kenyela.
Lukius alitoa taarifa kituo cha Polisi Wazo Hill, Mei 15 mwaka huu, siku ambayo tukio lilitokea na kupewa RB namba 3607/2013.
http://www.mtanzania.co.tz
0 comments:
Post a Comment