BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MNYAMA DUMA AMNG'ATA RAIS BOTSWANA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZxz7XxAmSpyMexcz3py7MGf3qFBvoomNRiRkyIsB5eeEmvF2BGU3tuz03GuSl3e5G3FXkI11E5y_0hCYvqzNohRaK2h_0sM4sjrkMWKz0puh8axUB3kAedM4kFk3TdoNrFIUsxvggyb8/s1600/asiatic_cheetah%255B1%255D.jpgDUMA AKIWA KATIKA MAWINDO.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiQI9Ms7kRfkpapD8jBLy2AYSvqw0Isy8AoQVqiUZ_4aUR7udLs1QXEEW6ZPYIHSSAT0iv8jNn_DCz-astYEbfPaevv138ABINo75_hFB6Z0ONgZ1KU5EIDlim3SkOgSiVgSLmRT3xOS4/s640/Ashambuliwa+na+duma+wa+kufuga+1.jpgDUMA AKIMSHAMBULIA BINADAMU.130429123248_khama_304x171_302_nocredit[1]RAIS wa Botswana, Ian Khama ameshonwa nyuzi baada ya kung'atwa na Duma kwa mujibu wa maafisa wakuu wa nchi hiyo.

Mnyama huyo alikuwa analishwa chakula alikokuwa anahifadhiwa katika kambi ya kijeshi wakati alipomrukia rais Khama na kumgwara.

Tukio hilo ilikuwa ajali tu wala sio shambulio kali kwa mujibu wa msemaji wa serikali Jeff Ramsay aliyezungumza na waandishi wa habari.

Majeraha ya Khama yalikuwa madogo wala haikujitokeza kama ajali kubwa.

Inaarifiwa ajali ilitokea ghafla na kumgutukia Rais Khama na walinzi wake.

"Duma alimgwara tu lakini sio ku
mshambulia kama wanavyodahani watu wengi,'' alisema bwana Ramsay.

Bwana Khama alionekana akiwa amevalia plaster kwenye mkutano ulioandaliwa baada ya tukio hilo.

Duma, ambao ndio wanyama wenye kasi kubwa zaidi ardhini, ni moja ya wanyama wanaokabiliwa na tisho kubwa la kuangamia.

Ni wanyama 12,400 pekee wanaosemekana kusalia mbugani katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Botswana. Tukio ambalo lilitokea April mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: