Mshambuliaji wa Yanga, Didie Kavumbagu akimgonga kwa kiwiko mwamuzi,
Martin Saanya aliyejaribu kuzuia asipigane na beki wa Simba Masoud
Nassor ‘Cholo’ na Kocha Patrick Liewig. Picha na Jackson Odoyo.
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Didier Kavumbagu amemtaka radhi mwamuzi Martin Saanya kutokana na kumgonga na kumsababishia maumivu makali alipokuwa akijaribu kumzui asipigane na beki wa Simba SC, Nassor Masoud ‘Cholo’ juzi Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa.
Wachezaji hao wawili walitaka kupigana baada ya
kutofautiana katika dakika za mwisho za mche
zo huo uliomalizakwa Yanga kwa kushinda mabao 2-0.
zo huo uliomalizakwa Yanga kwa kushinda mabao 2-0.
Akizungumza na Mwananchi jana
Kavumbagu alisema kuwa hakukusudia kumuumiza mwamuzi huyo isipokuwa
alimgonga kwa bahati mbaya wakati tulipotofautiana na Cholo.
“Hata hivyo baada ya tukio hilo nilimtaka radhi,
pia baada ya mechi kumalizika likwenda kumwona alipokuwa amepumzika
katika chumba cha tiba ndani ya Uwanja wa Taifa na nikamwomba msahama
kwa mara nyingine tena,” alisema Kavumbagu.
Katika hatua nyinge mshambuliajo huyo wa kimataifa
wa Burundi alisema hana ugomvi wowote na Cholo ila kitendo lilichotokea
uwanjani pale ilikuwa ni hali ya mchezo ambayo mchezaji yeyote anaweza
kufanya.
Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki
wengi wa soka hapa nchini Kavumbagu alifungia Yanga bao la kwanza kabla
ya Hamis Kiiza kupachika wavuni bao la pili na kuwanyamazisha kabisa
mashabiki wa Simba.
0 comments:
Post a Comment