HALI bado haijatulia
katika Mji Mtwara baada ya vipeperushi zaidi na ujumbe mfupi wa simu
kusambazwa katika kila kona ya mji huo kuwataka wananchi leo kutofanya
kazi wala kufungua biashara ili wasikilize mjadala wa hutuba ya Wizara ya
Nishati na Madini ya mwaka wa fedha ya 2013/2014 kama itakubali ‘Gesi ITOKE’ au
la.Mmoja wa waandishi wa habari alisema kwamba watu wamehamasishana kufanya hivyo kesho (leo) ili kuonyesha kwamba bado wanalisimamia suala hilo.
“Hali siyo nzuri, watu wamehamasishana kesho (leo) kutokufanya kazi,” alisema mwandishi huyo.
Ujumbe unaosambazwa katika simu za mkononi unasema: “ Waziri wa Nishati na Madini amegah
iri kuzungumzia bajeti ya Nishati na Madini kwa siku nne, ina maana mpaka jumatanoleo
“Kwa hiyo kama unashughuli ya kufanya ifanye ili Jumatano usifanye kwa sababu machafuko ambayo yanataka kutokea si ya kawaida.
Tafadhali wafahamishe watu wa kusini wote ambao wanataka mabadiliko. Tusiache kauli yetu, ‘gesi kwanza, uhai baadaye’.
“Hii ni kwa wakazi wote wanaoishi mikoa ya Kusini.. kuanzia vijiji na wilaya zote, tunakumbusha kuwa siku ya Jumatano Mei 22, 2013 kuanzia saa 3:00 asubuhi tusikilize Bunge juu ya uwasilishwaji wa bajeti ya Nishati na Madini.. tujue hatma yetu wana kusini kuhusu gesi yetu.
“ Kama kawaida yetu siku ya hiyo hakutakuwa na kazi, huduma zote za jamii zisitishwe kuanzia bobaboda , maduka, daladala hata gari za mikoani.
“Onyo , ukikutwa umekiuka agizo la wana kusini kazi kwako. Tuma ujumbe huu kwa wana kusini wote… gesi haitoki hata kwa bomba la peni.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa amesema kwamba atafanya
uchunguzi kuhusiana na suala hilo.Wakazi wa Mtwara wanashinikiza Serikali itamke kwamba GESI HAITATOKA na badala yake itabaki Mtwara kwa ajili ya kuwanufaisha kama vila vijana kupata ajira.
Awali baada ya kutokea vurugu na kusababisha vyumba kuchomwa moto na kuharibu mali mbalimbali, serikali ilitangaza kwamba Mtwara kutajengwa kiwanda kikubwa cha saruji ambacho kitawanufaisha wananchi wa mkoa huo.
Serikali ilisema vijana watapata ajira na kutajengwa pia kiwanda cha ku-process gesi kabla ya kusafirishwa Dar es Salaam na hivyo kutoa ajira na kuimarisha uchumi wa mikoa ya Kusini.

0 comments:
Post a Comment