BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NEWS ALERT:MWANAFUNZI CHUO KIKUU AJINYONGA.

Mwanfunzi wa Chuo Kikuu aliyejinyonga Yobe Magongoninga Mfune (23) 



Lilongwe,Malawi
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Bunda kilichopo mijini Lilongwe nchini Malawi, amejinyongwa kwa kutumia mkanda wa begi lake la kusafiria. Mwanfu
nzi huyo aliyetambulika kwa jina la Yobe Magongoninga Mfune (23) alikatisha maisha yake huku sababu za kifo cha kikiwa siri kati yake na Mungu wake.

Akizungumza na Mwandishi wa habarimpya.com, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Malawi Rhoda Manjolo alisema kwamba, Mfune alikuwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika fani ya utawala wa mazingira na maliasiri.

Manjolo alisema, marehemu alikutwa amejinyonga katika chumba chake kwenye hosteli za chuo hicho. Hata hivyo Polisi walisema kwamba, marehemu alikuwa na mahusiano na mwanamke mmoja aliyewahi kufanyakazi katika chuo hicho kwa siku za nyuma.

Msemaji wa Polisi nchini Malawi aliongeza kwamba, marehemiu alikuwa akiishi na rafiki yake katika chumba hicho ambaye aliondoka tangu may 6 mwaka huu na aliporudi akakuta mlango umefungwa kwa ndani ndipo alipoamuwa kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo ambao waliamuwa kuvunja mlango huo kuingia ndani.

Alisema kwamba baada ya mlango huo kufunguliwa hawakuona mtu lakini walipofungua kabati la nguo wakakutana na mwili wa marehemu ukiwa unaning'ining'ia. "Uchunguzi wa madaktari unasema kwamba kifo cha mwanafunzi huyo kilitokana na msongo wa mawazo"alisema Manjolo.

Hata hiyo marafiki wa karibu wa mwanafunzi huyo walisema kwamba, siku chache kabla ya marehemu kufariki dunia aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa Face Book kwamba "nitaweka historia nyingine mpya ambayo sijawai kuiweka tangu nilipozaliwa, na kumbukukumbu yake haitakaa ikafutika tena,na baada ya hapo sitajali wala kuwa na mahusiano na mambo yote ya hapa duniani, bali itakuwa juu yangu na Mungu wangu"ilisema sehemu ya status za marehemu.
Habari hii imeandaliwa Gace Banda mwakilishi wa habarimpya.com nchini Malawi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: