Kwa ufupi
Nitapenda kuona Rais Kikwete akikataa jambo
hilo kwani litachafua taswira ya nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala
bora,” alisema Profesa Lipumba.http://www.mwananchi.co.tzRAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE.
DAR ES SALAAM.
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amedai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serik
ali ya sasa kukaa madarakani.
Profesa Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi
kuwa mchakato wa Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo
kutokuwa rahisi kwa uchaguzi kufanyika mwaka 2015.
Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati akifungua
kikao cha Baraza Kuu la CUF, Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali
inataka kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha
kuwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa
madarakani hadi mwaka 2017.
Hata hivyo, madai hayo ya Profesa Lipumba
yamepingwa vikali na Serikali na viongozi wake watatu waandamizi ambapo
walijibu walipoulizwa kwa maandishi na mwandishi wetu mjini Dodoma
wanakohudhuria kikao cha Bunge.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe
alijibu: “Mchakato wa Katiba upo ‘on track’ (unakwenda vizuri) hatuna
sababu ya kufanya hivyo.”
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijibu” “Njooni ofisini kwangu nitasema ni kitu gani.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Uratibu na Bunge, William Lukuvi alijibu kwa utani bila ya kufafanua:
“Njooni niwajuze, unajua kamba haitoki Ukambani kama ilivyo kamba.”
Profesa Lipumba amemwomba Rais Kikwete asilikubali
wazo hilo akisema wananchi hawatakubali na taifa linaweza kuingia
katika mtafaruku.
“Nitapenda kuona Rais Kikwete akikataa jambo hilo
kwani litachafua taswira ya nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala
bora,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema Serikali haipaswi kuhofia uchaguzi kwa
sababu ya Katiba kwani bado uwezekano wa kuandaa uchaguzi wa haki na
huru unawezekana kwa utaratibu mwingine.
“Mchakato wa Katiba unaendelea, Tume ya Mabadiliko
ya Katiba inatuambia kwamba mwaka 2014 tutakuwa na Katiba Mpya, sasa
CUF tunasema kwamba hata kama Katiba Mpya haitapatikana kwa kipindi
hicho kuwe na Tume huru ya Uchaguzi,” alisema Profesa Lipumba.
Jukwaa la Katiba kutinga mahakamani.
0 comments:
Post a Comment