Kwa ufupi
Hakuna barabara kwangu, kwa nini niunge mkono
hoja? Namshangaa sana Kapuya kwa tabia aliyonionyesha pale... Mbona mama
Margaret Sitta amesema Tabora hakuna barabara hawakumfuata ?. http://www.mwananchi.co.tzMbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy kushoto akibishana na wabunge wa CCM ambao walimlalamikia kwa kuipinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi jana. kutoka kushoto ni Mendrady Kigola (Mufindi Kusini) na Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi) katika viwanja vya bunge mjini Dodoma, Picha na Edwird Mjwahuzi.
DODOMA.
WABUNGE wa CCM, jana walizua tafrani nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kukasirishwa na kitendo cha mwenzao wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy kupinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
WABUNGE wa CCM, jana walizua tafrani nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kukasirishwa na kitendo cha mwenzao wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy kupinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Katika mchango wake, Keisy alisema haungi mkono
hoja kwa sababu Barabara ya Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni
haijajengwa kwa kiwango cha lami.
Alisema zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya
ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya
ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
Mara baada ya Bunge kuahirishwa, Keisy akiwa nje
ya ukumbi huo alifuatwa na Mbunge wa Urambo Mashariki, Profesa Juma
Kapuya, Omary Nundu (Tanga Mjini), Mendrady Kigola (Mufindi Kusini) na
Rita Kabati (Viti Maalumu) na kumzonga.
Baada ya wabunge hao kumzonga, Profesa Kapuya
ambaye amewahi kuwa waziri serikalini alihoji kitendo cha mbunge huyo
kupinga bajeti... “Kwa nini umekataa kuunga mkono hoja? Ulikuwa
unalidanganya Bunge wakati unachangia si kweli huko Rukwa hakuna
barabara, barabara mnazo.”
Kessy alionekana kukerwa na swali hilo na kumjibu
kwa hasira: “Nyinyi na mimi nani ni mbunge Nkasi? Mimi sina unafiki
napinga kutokana na yaliyopo jimboni kwangu sipo hapa bungeni
kuwafurahisha nyinyi na wala Serikali. Nipo kwa masilahi ya wananchi
wangu.” Baada ya majibu hayo, mbunge huyo aliondoka haraka eneo hilo.
Baadaye jioni mwandishi wetu alimfuata ili kupata
ufafanuzi juu ya msimamo wake... “Hakuna barabara kwangu, kwa nini
niunge mkono hoja? Namshangaa sana Kapuya kwa tabia aliyonionyesha
pale... Mbona mama Margaret Sitta amesema Tabora hakuna barabara
hawakumfuata ?.”
Alisema wabunge hao hawana haki ya kuhoji kwa nini
hakuunga mkono hoja kwa kuwa kila mmoja amekuja bungeni kutokana na
kushinda katika jimbo lake. Akichangia hotuba ya bajeti hiyo, Kessy
alisema haungi mkono hoja kwa asilimia 100 hadi pale atakapoelezwa lini
barabara hizo zitajengwa.
Alisema zaidi ya vijiji 30 vya mwambao wa Ziwa
Tanganyika na Barabara ya Kipili hadi Bandarini ni mbovu kwa kiasi
kikubwa na muda wake wa ujenzi kumalizika umeshapitiliza miezi mitatu
iliyopangwa.
Alisema nchi imegawanyika kwani baadhi ya majimbo
ya wabunge yana lami hadi mlangoni lakini Nkasi hawajawahi kuiona akitoa
mfano wa Jimbo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Mpanda Mashariki) Same
Mashariki kwa Anna Kilango.
0 comments:
Post a Comment