Wameondoka pamoja; Marafiki Ngwea kushoto na M enzi za uhai wao.
WAKATI
rafiki wa msanii Albert Mangwea, M To The P naye amefariki dunia
asubuhi ya leo nchini Afrika Kusini, familia ya marehemu tayari imeanza
taratibu za mazishi.
Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, alifariki dunia jana jio
ni akiwa nchini Afrika Kusini.
Inadaiwa
Ngwair alifariki dunia kutokana na kuzidiwa na matumizi ya dawa za
kulevya na wakati mwili wake unakimbizwa hospitali ya St Hellen Joseph,
rafiki yake naye, msanii pia M To Te P alikuwa katika hali mbaya, pia
kwa utumiaji wa dawa za kulevya.
Taarifa kutoka Afrika Kusini, zimesema swahiba huyo wa Ngwair naye amefariki dunia.
Kaka
wa marehemu Ngwair, Kenneth Mangwea amesema msiba upo Mbezi Beach,
Goigi mjini Dar es Salaam na taratibu za kuirejesha miili ya marehemu
nyumbani zimeanza.
Tayari
vifo vya wasanii hao wawili vimeanza kuzalisha maswali magumu, kubwa
likiwa ni utumiaji wa dawa za kulevya pekee ndio umesababisha vifo vyao,
au kuna mambo yaliyojificha.
Kimuziki,
Ngwair aliibukia mkoani Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Dark
Master, Noorah na Mez B na amekuwa akishirikiana na M To The P tangu
akiwa msanii anayechipukia baada ya kuhamia Dar es Salaam.
Baada
ya kuja Dar es Salaam, Ngwair akapata dili Bongo Records chini ya
mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi
kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.
Wimbo
wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia
umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003
ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.
Hata
hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa
dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa
usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo
gari aina ya Jeep.
Ngwair
kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam
akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu
mbalimbali Dar es Salaam.
Mwaka
2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu
kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na
kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.
Hata
hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo
hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na
‘kuharibika zaidi’.
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
Mwaka
2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka
na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho
alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz.
Ngwair
alijaribu sana kumuinua kimuziki M, lakini pamoja na ukweli kwamba
alikuwa ana kipaji, lakini hakufanikiwa, ingawa aliwahi kutoa albamu.
Pumzikeni kwa amani. Mbele yenu, nyuma yetu. RIP.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment