BannerFans.com BannerFans.com

ALBERT MANGWEA KUZIKWA MOROGORO ALIKOZIKWA BABA YAKE.

No Comments


 
KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa na baba yake mdogo kupitia East Africa Radio leo asubuhi, mazishi ya rapper Albert Mangwea aliyefariki jana katika hospitali ya St. Helen jijini Johannes
burg, Afrika Kusini yanaweza kufanyika mjini Morogoro.“Tumekubaliana kwamba tumelazimika kuzika Morogoro kwasababu huyu kaka yetu ambaye ni baba wa marehemu tumemzika pale Morogoro na familia yote ya marehemu ipo pale Morogoro. 

Lakini hapa Dar es Salaam tutafanya mapokezi na msiba utakuwa hapo kwa kaka yangu ni sehemu za Mbezi hapo, kwahiyo tutakuwa kwa kaka yangu anaitwa David Mangwea,” amesema.

Ameongeza kuwa taarifa hizo za msiba nao walizipata jana jioni lakini bado hawajawa na uhakika ni vipi mwili wa marehemu utaletwa nchini kutokea Afrika Kusini.

“Kitu tunachokifanya na tumewaagiza tu hao vijana wetu waliopo hapo Dar es Salaam wajaribu kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini kuona namna gani ambavyo tunaweza kupata more information na kiasi kwamba tukaweza kujua namna gani msiba utakuja hapa.”

Mpaka sasa bado haijajulikana mwili wa marehemu Mangwea utakuja lini nchini.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home
Post a Comment