BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RIPOTI YA DAKTARI YAONYESHA ALBERT MANGWEA AMEFARIKI KUTOKANA NA ‘DRUG OVERDOSE’


l
DAKTARI Shirley Radcliffe wa hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini, amethibitisha kwenye ripoti yake kuwa Albert Mangwea amefariki kutokana na “alcohol toxicity” (Alcohol intoxication ni hali inayo
tokana na matumizi makubwa ya pombe). 

Hiyo ni baada ya Mangwea kunywa sana pombe, kuchoka kupita kiasi na kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi


Inasemekana kuwa Albert, 28, alianguka nyumbani kwa marafiki zake na alikuwa amekunywa pombe zaidi ya mara tano ya kinachotakuwa kunywewa nchini Afrika Kusini ambapo kwenye damu yake kulipatikana 416mg za pombe kwenye kila milliliters 100. 

Radcliffe ameeleza kuwa sababu ya Ngwair kupelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ni pamoja na hypoxia (upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tissue za mwili) na mmoja wa marafiki zake alipatikana na chumba mbili tupu za Vodka ziizokuwa kwenye gari. 

Ripoti hiyo inadai kuwa Ngwair alikuwa na tatizo la kutokula chakula miezi kadhaa kabla ya kifo chake na pia kujirusha bila kupumzika hata kidogo. 

Sampuli zilizopatokana tumboni mwake zimeonesha mkusanyiko wa madawa ya kulevya mbalimbali yakiwemo Heroin,Cocaine ‘crack’ na bangi ya 0.08gms ilipatikana kwenye damu yake.

Kifo chake kilitokana na na mshtuko mkali wa moyo na kushindwa kupumua kulikotokana na moyo kuacha kufanya kazi na hivyo kupelekea kifo chake ndani ya sekunde chache tu.

Muda mfupi uliopita tumetoka kuzungumza na Soggy Doggy, Noorah, Mwana FA na Cpwaa kuhusu jinsi walivyokuwa karibu na Albert Mangwea wakati wa uhai wake. Soggy pia amemzungumzia M to The P ambaye naye ‘inasemekana’ amefariki. 

Wote walipelekwa wakiwa mahututi kwenye hospitali ya St. Helen nchini Afrika Kusini. Soggy aliishi na M to The P kwenye chumba chake kwa mwaka mzima. 

Kuna mengi usiyoyafahamu kuhusu Ngwair utayasikia kwenye sauti hizi.
 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: