Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge
Mutahaba.
IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa
Habari Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani
kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media
Group Ruge Mutahaba na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith
‘Wambura Lady Jaydee’ Ruge ametoa ya moyoni.
Mwandishi wa habari hii alimpigia simu Ruge na
kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutam
ka kwamba atawaita wawili hao
na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kama nilivyosema katika tamko langu wiki
iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote
mbili hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi
sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa
kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama
kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize
maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi
kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huo huo Ruge ameongeza kwamba tayari
ameshatoa fuara taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungua jalada la
malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa msanii
huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza
kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la
mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka
na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama
facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo
ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumla
tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady
Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mume wake Gadner
Habash simu iliita bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment