BAADA ya Lady JayDee kusema amepokea habari ambazo alikuwa bado
hajazidhibisha kuwa anatakiwa mahakamani na kuomba kama ni kweli isiwe
tarehe ambayo anafanya show ya miaka 13 ya Lady Jaydee, sasa inaonekana
amesha confirm kuwa anatakiwa kufika mahakamani jumatatu ya tarehe 13
May mwaka huu.
Jide amewapa
fans wake taarifa jana jioni kupitia facebook na twitter kuhusu
kufikishwa kwake mahakamani na kwamba ataendelea kuwajuza
kinachoendelea.
“Ratiba ya Usiku wa leo ni
MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya
Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea.
Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk asubuhi.
0 comments:
Post a Comment