Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa
wakuu na wamiliki wa shule na vyuo binafsi kwa minajili ya kuboresha
sekta ya elimu haoa nchini.
Akizungumza
na viongozi wa TAMONGSCO Rais Kikwete amesema sekta binafsi ina
mchango mkubwa wa kuinua elimu hapa nchini hivyo jitihada za pamoja
zinahitajika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza
Rais
Kikwete aliwataka wamiliki na wakuu wa shule na vyuo binafsi kupunguza
ada kubwa wanazotoza kwa wanafunzi ili watanzania wengi hasa wa kipato
cha chini waweze kupata fursa ya elimu.
Aidha
Mheshimiwa Rais alisema serikali iko katika Mchakato wa kutunga Sera
Mpya ya Elimu baada ya ile ya mwaka 1995, umefi
kia katika hatua za mwisho na kinachosubiriwa sasa ni maoni ya Wabunge ili Sera hiyo ikamilishwe na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.
kia katika hatua za mwisho na kinachosubiriwa sasa ni maoni ya Wabunge ili Sera hiyo ikamilishwe na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.
Wakati
huo huo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Taasisi ya Elimu
Tanzania itaanza maandalizi ya kupitia upya mitaala ya elimu nchini ili
nayo ilingane na malengo ya Sera Mpya ya Elimu,mahitaji ya maendeleo
nchini na duniani kwa ujumla.
Licha
ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu serikali kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali wa elimu imeongeza sekta hiyo ambapo kuna wanafunzi
zaidi ya milioni nane katika shule za msingi,zaidi wanafunzi milioni
moja na laki nane kwa shule za sekondari na zaidi ya laki moja na
sitini elfu kwa upande wa vyuo vikuu.
0 comments:
Post a Comment