
Amesema mbinu hiyo mpya imeanza kutumiwa na majangili hao kwa muda mrefu sasa na kwamba hivi sasa hawasafirishi pembe hizo zikiwa nzima nzima kwa kuwa watakamatwa na vyombo vya usalama.
Mbowe ameliambia Bunge kwamba hivi sasa, meno hayo hayasafirishwi tena kwa meli kama zamani na badala yake kuna viwanda nchini ambavyo vinasaga meno hayo na kisha kusafirishwa kama unga kupitia viwanja vya ndege vya Tanzania.
Amefafanua kwamba mtandao wa ujangili nchini unakua kila siku na kwamba watu wanaofanya biashara hiyo wapo karibu na baadhi ya viongozi wa serikali na wanajulikana na vyombo vya usalama.
Pamoja na kutaja kwamba kuna kiwanda cha kusaga pembe za ndovu, Mbowe hakukitaja kiwanda hic
ho.
Kamati ya inayoshulika na masuala ya maliasili na utalii ya serikali na ambayo inaongiozwa na wabunge imesema kwamba miaka saba ijayo tembo wote watakuwa wamemalizika endapo serikali haitachukua hatua kali za kuthibiti majangili wanaoihujumu sekta hiyo.
Mbowe ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya maliasili na utalii ya mwaka wa fedha 2014/14.
Wakati akichangia Mbowe ameitaka serikali kuchukua hatua kali ili kudhibiti majangili wa pembe za tembo kwa kuwa watu hao wabaya ambao wanaliangamiza taifa.
“ Mheshimiwa mwenyekiti, naomba serikali ichukue hatua kali ikiwezekana serikali majangili wote wanaohusika wanyongwe, wote wanyongwe, adhabu hiyo itasaidia kukomesha mauji ya tembo wetu.
0 comments:
Post a Comment