Kwa ufupi
Uamuzi huo wa Serikali umetokana na matokeo mabaya
ya mitihani huo yaliyosababisha zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi kupata
sifuri.http://www.mwananchi.co.tzWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KIGURUNYEMBE ILIYOPO MANISPAA YA
MOROGORO WAKIFANYA MTIHANI WA TAIFA SOMO LA KISWAHILI SHULENI HAPO MWAKA 2012.
PICHA NA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi, akiwasilisha kauli ya serikali Bungeni Dodoma jana kuhusu
taarifa ya awali ya Tume ya Taifa ya kuchunguza matokeo ya mtihani wa
taifa wa Kidato cha nne wa mwaka 2012. Picha na Edwin Mjwahuzi.
DODOMA/DAR.
SERIKALI imechukua uamuzi mgumu na kuamua kuwafariji wanafunzi waliofeli mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka 2012 baada ya kufuta matokeo hayo na kuamua yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011.
Uamuzi huo wa Serikali umetokana na matokeo mabaya
ya mitihani huo yaliyosababisha zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi
kupata sifuri.
Kutokana na matokeo hayo, Serikali iliunda Tume
inayoongozwa na Profesa Sifuni Mchome kuchunguza matokeo hayo ili kupata
ufumbuzi wa kudumu.
Muda mfupi baada ya tamko la Serikali, baadhi ya
wadau wa elimu wameeleza kufurahishwa na uamuzi huo, huku Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) kikiikosoa hatua hiyo, kuwa imekiuka sheria na
kupora madaraka ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
Akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu taarifa ya
awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Mtihani wa Taifa Kidato
cha nne mwaka 2012 jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu
na Bunge), William Lukuvi alise
ma wameagiza Necta kuweka viwango ili matokeo ya wanafunzi yalingane na juhudi zao.
ma wameagiza Necta kuweka viwango ili matokeo ya wanafunzi yalingane na juhudi zao.
“Standardization ifanyike ili matokeo ya wanafunzi
yalingane na juhudi wazizoziweka katika kusoma kwa mazingira, hali
halisi ya Tanzania na uamuzi wa taifa kuongeza idadi ya shule na
wanafunzi wakati uwekezaji katika ubora unaendelea,” alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema Necta imeelekezwa kuwa licha ya
sheria ya kuanzishwa kwake kuruhusu kufanya marekebisho ya mchakato wa
mtihani, marekebisho yoyote ya kubadilisha utaratibu wa kupanga viwango
vya ufaulu na madaraja ya mitihani yanatakiwa yahusishe wadau wote
wanaohusika na mitalaa, ufundishaji na mtihani.
“Wakati Tume inaendelea kukamilisha kazi yake,
uamuzi wa Necta kutumia utaratibu mpya wa kupanga viwango vya ufaulu na
madaraja ya matokeo ya mitihani uliotumika 2012 usitishwe,” alisema
Lukuvi na kuongeza:
“Badala yake Necta itumie utaratibu uliotumika
mwaka 2011 kwa kidato cha nne na sita kwa mitihani yote, ikiwamo
utaratibu wa Standardization na kutoa matokeo mapya kwa kuzingatia
maelekezo haya.”
Pia, Serikalli imeagiza mchakato wa tuzo wa taifa
(National Qualifications Framework) na Mfumo wa Kutahiniwa/ kuthamini
maendeleo ya mwanafunzi masomo yake (National Assessment Framework)
ukamilishwe haraka iwezekanavyo.
Katika mtihani wa mwaka 2012, wanafunzi 367,756
walifanya mtihani huo na waliofaulu ni 126,847. Waliofaulu kwa kwa
madaraja ya kwanza hadi la tatu ni 23,520 sawa na asilimia 6.4 na daraja
la nne ni 103,327 sawa na asilimia 28.1, huku 240,909 ambao ni asilimia
65.5 wakipata daraja sifuri.
Kauli ya CWT
0 comments:
Post a Comment