BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHEIKHE ISSA PONDA APATIKANA NA HATIA, AFUNGWA KIFUNGO CHA NJE MWAKA MMOJA.

http://www.mwananchi.co.tz


DAR ES SALAAM.  
FURAHA zilitawala jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda Issa kuhukumiwa kifungo cha nje cha miezi 12 huku wenzake 49 wakiachiwa huru.
Katika kesi hiyo, Sheikh Ponda na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni, uchochezi na kuingia kwa jinai katika ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali.
Katika hukumu hiyo, Mahakama ilimhukumu Sheikh Ponda kifungo hicho cha nje kwa kosa moja la kuingia kwa nguvu katika eneo hilo la ardhi isiyo yake.
Hukumu hiyo iliwaachia huru washtakiwa wenzake wote baada ya kuridhika kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.
Kabla ya hukumu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alisema upande wa Jamhuri hauna kumbukumbu za makosa mengine ya jinai dhidi ya mshtak
iwa lakini akaiomba Mahakama impe adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria.
Akitoa hukumu hiyo iliyosomwa kwa saa 2:12, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Victoria Nongwa Nongwa alisema: “Kwa kuwa mshtakiwa hana rekodi ya makosa ya jinai na kwa kuwa amekaa rumande kwa muda mrefu baada ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) kuzuia dhamana yake, ni haki kuangalia muda huo.”
“Hivyo Mahakama chini ya Kifungu cha 25(g) cha Kanuni za Adhabu, mshtakiwa unaachiwa kwa masharti ya kutokutenda kosa kwa miezi 12. Unatakiwa ulinde amani na kuwa na tabia njema katika jamii. Ukishindwa hiyo utarudi hapa kwa adhabu nyingine inayokufaa.”
Awali, Hakimu Nongwa alichambua ushahidi wa mashahidi wote 16 wa upande wa mashtaka na 53 wa utetezi akasema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.
Alisema umeshindwa kuthibitisha katika kosa la kwanza, la tatu na la nne, yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa wote na katika shtaka la tano lililokuwa likimkabili Sheikh Ponda na Mshtakiwa wa tano, Sheikh Mukadam Swalehe ambaye ni Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu.
Katika shtaka la pili, Hakimu Nongwa alisema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa wa kwanza tu, Ponda na kwamba kwa upande wa washtakiwa wengine umeshindwa kuiridhisha Mahakama kuwa walitenda makosa hayo.
Alisema hakuna ushahidi unaoonyesha jinsi washtakiwa hao walivyohusika katika makosa.

Hata hivyo, kwa upande wa mshtakiwa wa tano japo kuna maelezo ya onyo yanayoonyesha kuwa alikiri, lakini akasema maelezo ya onyo tu ya mshtakiwa hayatoshi kumtia hatiani, bali upande wa mashtaka ulipaswa kuweka wazi suala hilo.

Hakimu Nongwa aliponda upelelezi kuwa haukufanyika kwa umakini kiasi kwamba kuna mambo ambayo hayakuwa wazi yaliyoibuliwa na upande wa utetezi, ambayo kama upelelezi ungefanyika kwa umakini, washtakiwa wote wangetiwa hatiani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: